Wakazi wa Kiambu wakadiria hasara kutokana na hitilafu za umeme zinazoteketeza nyumba zao

Wakazi wa mtaa wa Kiamumbi katika mji wa Kiambu wameelezea wasi wasi wao kutokana na visa vingi vya kuteketea kwa nyumba kutokana na hitilafu za umeme.

Haya yanajiri baada ya nyumba moja kuteketea wakati umeme uliporejea baada ya kupotea kwa kipindi kirefu.

Aidha wamesema vifaa kadhaa vya kielektroniki vilichomeka katika nyumba zilizo jirani na nyumba hiyo.

Also Read
Waziri Kariuki asisitiza umuhimu wa maji katika maendeleo nchini

Kulingana na Musa Muchendu, ambaye nyumba yake iliteketea, kupotea kwa umeme kumekithii katika sehemu hiyo na umeme unaporejea husababisha uharibifu kwa vifaa vya nyumbani vinavyotumia umeme.

Muchendu alisema ni jukumu la kampuni ya Kenya Power kuhakikisha inatoa kiasi kinachohitajika cha umeme na kuwafidia waliochomekewa na vifaa vyao vya nyumbani kutokana na hitilafu za umeme.

Also Read
Polisi Abaka Binti Aliyekwenda Kushtaki Ubakaji India

Alisema amepoteza vifaa vingi vya umeme kwenye mkasa huo.

Aidha mkazi mwingine wa sehemu hiyo, John Ngata, aliitaka kampuni tya Kenya Power kushughulikia kasoro hiyo ili kuepusha hasara zaidi.

Also Read
Mwanasheria mashuhuri Nzamba Kitonga kuzikwa leo

Naye John Chege, ambaye pia ni muathiriwa mwengine, amesema wakazi wa eneo hilo huenda wakalazimika kutafuta mbinu mbadala za kupata umeme kama vile kutumia sola kutokana na kero za huduma za Kampuni ya Kenya Power.

  

Latest posts

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Maafisa wa Utawala waonywa dhidi ya kujihusisha na siasa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi