Wakazi wa Kisii wasusia hospitali, wajitafutia dawa ya Korona

Watu wa matabaka mbali mbali katika Kaunti ya Kisii wameamua kujitafutia wenyewe matibabu ya ugonjwa wa Korona, badala ya kutembelea taasisi zilizoidhinishwa za afya.

Habari zinaarifu kuwa hali hiyo ni kutokana na hofu kuwa wataambukizwa virusi vya Korona, au kupimwa na kuthibitishwa kwamba wameambukizwa virusi hivyo kisha wapelekwe katika vituo vya kuwatenga, ambako watashindwa kulipia gharama kubwa za hospitali.

Madaktari bandia wamefurahia hali hiyo na kuendeleza biashara haramu ya kuwapa dawa ambazo wanadai zinaangamiza virusi vya Korona, huku wakijipatia fedha nyingi kutoka kwa wakazi hao.

Also Read
Idadi ya wasichana wanaochanjwa dhidi ya maambukizi ya HPV yapungua nchini

Katibu Mkuu wa Baraza la Tamaduni na Maendeleo ya jamii ya Abagusii Bosire Angwenyi anaeleza kuwa ugonjwa wa COVID-19 unaathiri mapafu na anaeleza jinsi wakazi wanaojishuku na dalili za ugonjwa huo wnaavyojitibu.

Kulingana na Bosire, mizizi au majani ya miti Fulani huchemshwa kwenye chungu kilichofunikwa kisha mgonjwa anapumua kwenye mvuke huo.

Also Read
Wafanyibiashara Busia waitaka serikali kuwalipia ada ya NHIF

“Huo mvuke unauvuta, unaenda kwa mapafu unafungua kila kitu na unakuwa sawa kabisa na unaona mtu baada ya masaa machache anaanza kutembea,” anaeleza Bosire.

Bosire anaomba taasisi za utafiti wafanyie uchunguzi miti hiyo inayotumika akiwa na tumaini kwamba huenda ikaleta matokeo mazuri yanayoweza kusaidia Wakenya kutokana na ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa Afya ya Umma Kaunti ya Kisii, Dkt. Richard Onkware, ameonya kwamba Korona ni ugonjwa unaosambazwa kupitia kwenye hewa na ambao hauna tiba hadi sasa, akiongeza kuwa utafiti unafanywa ili kupata tiba kamili.

Also Read
Watalii wanaozuru Kilifi wahakikishiwa usalama wao

Hata hivyo, Onkware amesema ni sharti watu wote wafuate maagizo ya Wizara ya Afya ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Dk. Onkware ameashiria kwamba mipango inafanywa ya kunzisha kituo cha kupima watu kwenye Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii hivi karibuni, ili kuwaondolea tatizo la kupeleka sampuli jijini Kisumu.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi