Wakazi wa Laikipia Kaskazini wanufaika na kisima kutoka kwa wafadhili

Mbunge wa Laikipia kaskazini, Sarah Korere ameapa kuungana na wafadhili kuhakikisha wakazi wa eneo bunge lake wanakunywa maji safi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kisima ambacho ujenzi wake ulifadhiliwa na shirika la  Habitat for Humanity Germany kwa ushirikiano na shirika la Habitat for Humanity Kenya katika kijiji cha Kandutura, Korere alisema mengi yahitaji kufanywa kuhakikisha kuna maji katika eneo bunge hilo kame.

Also Read
Kaunti ya Elgeyo Marakwet yaangusha mswada wa BBI

Kisiwa hicho ambacho kinatarajiwa kuhudumia makazi 3,500 kitapunguza mzigo kwa wakazi ambao hapo awali walitembea mwendo wa kilomita 5 kutafuta bidhaa hiyo muhimu.

Korere alilipongeza shirika la Habitat kwa kuchimba kisima hicho cha gharama ya shilingi milioni 3.8 na kukiwekea mtambo wa umeme unaotumia miale ya jua ambao unaimarisha usambazaji maji katika eneo hilo.

Also Read
Marekani kuisaidia kaunti ya Mombasa kuboresha utoaji wa huduma

Afisa wa mipango wa shirika la Habitat humu nchini Nixon Otieno, alisema baada ya uzinduzi wa kisima hicho jamii ya sehemu hiyo inatarajiwa kudumisha kisima hicho kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Also Read
Kenya yalipiza kisasi kufuatia tangazo la Uingereza kutoruhusu abiria kutoka Kenya

Alisema pesa zinazopatikana kupitia uuzaji maji zitatumika kwa ukarabati wa kisima hicho.

Mtungi wa maji wa lita 20 unagharimu shilingi moja hatua ambayo itawezesha familia zisizojimudu katika eneo hilo kuweza kumudumu gharama hiyo.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi