Wakazi wa Magharibi mwa nchi wasifiwa kwa kukabiliana na Itikadi kali

Kamishna wa eneo la Magharibi mwa kenya, Esther Maina,amezipongeza jamii zinazoishi katika eneo hilo kwa kujitolea kukabiliana na itikadi kali.

Maina alisema siku za hivi majuzi wazazi wamekuwa wakiripoti visa vya mabadiliko ya tabia miongoni mwa watoto wao, na kutoweka kwao kutoka nyumbani kwa sababu zisizoeleweka, ili hatua za mapema zichukuliwe.

Also Read
Wakazi wa Laikipia Kaskazini wanufaika na kisima kutoka kwa wafadhili

Maina alikuwa akiongea wakati wa mafunzo kwa viongozi wa eneo hilo yaliyoandaliwa mjini kakamega na kituo cha kitaifa cha kukabiliana na ugaidi.

Alisema eneo la magharibi mwa kenya linatumiwa kuwaingiza humu nchini na kuwavukisha mpaka wafuasi wa makundi ya itikadi kali, kwa sababu kaunti za Bungoma na Busia ziko kwenye mpaka, hivyo basi ipo haja ya kuchukua hatua za pamoja kukabiliana na visa hivyo.

Also Read
Mpango wa Imarisha afya ya Mama na Mtoto wazinduliwa upya Kakamega

Maina alisema serikali itatoa mafunzo ya mbinu za kukabiliana na makundi hayo kwa machifu, manaibu wao na hata kwa wahudumu wa hoteli.

Also Read
Serikali kuwasaka wanafunzi ambao hawajajiunga na Kidato cha kwanza

Akiongea wakati wa mafunzo hayo, kamishna wa kaunty ya kakamega,Pauline Dola, alisema ipo haja ya kuwepo kwa ushirikiano kati ya polisi na vijana, ili waweze kubadilishana habari za usalama.

  

Latest posts

Uchaguzi wa Ugavana kaunti ya Mombasa na Kakamega umeahirishwa

Tom Mathinji

Gavana mteule wa Meru Kawira Mwangaza ajiunga na Kenya Kwanza

Tom Mathinji

Ruto: Nitawahudumia Wakenya wote kwa usawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi