Wakazi wa Mavoko, Kaunti ya Machakos, walalamikia uharibifu wa mazingira

Wakazi wa Eneo Bunge la Mavoko, Kaunti ya Machakos, wamelalamikia uvundo wa maji machafu yanayopitia katika vijiji vyao.

Wakazi hao wanasema Halmashauri ya Kitaifa ya Kuutunza Mazingira, NEMA, imeshindwa kudhibiti shughuli za kiwanda kinachomwaga maji machafu katika sehemu hiyo.

Also Read
Watu watano wafariki katika ajali ya barabarani Makueni

Wakazi hao wamedai kuwa watoto wamekuwa wakiambukizwa magonjwa ya ngozi, homa ya matumbo na maradhi mengine yanayoambukiwa kupitia kwa maji machafu kufuatia uharibifu mkubwa wa mazingira.

Also Read
Wakazi wa Machakos wahimizwa kuzingatia masharti ya kudhibiti Covid-19

“Watoto wanaokota takataka za kuchezea, wanashika shika uchafu mwingi hapa. Hatuoni mtu wa kushughulika,” amesema Nancy ambaye ni mmoja wa wakazi hao.

Kadhalika wanailaumu serikali ya Kaunti ya Machakos kwa kutozoa mirundiko ya takataka zinazotupwa kando ya barabara ambazo huhatarisha maisha yao.

Also Read
Rais Kenyatta amwomboleza mzee Edward Kiprotich Karoney

Wakazi hao wameipa serikali makataa ya wiki mbili kuokota mirundiko hiyo ya takataka na wametishia kuandamana iwapo matakwa hayo hayatatekelezwa.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi