Wakazi wa Mbeere kunufaika na mradi wa shilingi milioni 220 wa unyunyiziaji maji

Serikali ya kitaifa imezindua mradi wa unyunyiziaji maji mashamba kwa gharama ya shilingi milioni 220 katika eneo kame la Mbeere, Kaunti ya Embu.

Mradi huo wa Kanyuambora unaofadhiliwa na serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na halmashauri ya unyunyiziaji maji mashamba unatarajiwa kukamilika katika muda wa mwaka mmoja na nusu.

Also Read
Maafisa 11 wa usimamizi mtihani wakamatwa kwa udanganyifu

Waziri wa Maji Sicily Kariuki alimuagiza mkandarasi anayetekeleza mradi huo, Joycott General, kuhakikisha unakamilika kwa wakati ufaao.

Also Read
Waziri Kariuki asisitiza umuhimu wa maji katika maendeleo nchini

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Kariuki amesema utawafaidi wakazi 1,250 wanaokumbwa na tisho la njaa kutokana na ukame wa mara kwa mara.

Also Read
Sonko afikishwa mahakamani Kiambu na kukanusha mashtaka ya kuzua vurugu

Pindi utakapokamilika, wakulima wataweza kupanda mimea kama vile mahindi, mipaipai, vitunguu, nyanya na mingineyo itakayowaletea mapato.

Kariuki amesema wakazi zaidi watajumuishwa kweye awamu ya pili ya mradi huo.

  

Latest posts

Wakazi wa Nandi ya kati wahimizwa kushirikiana na polisi kukabiliana na uhalifu

Tom Mathinji

Serikali yahimizwa kutoa mikopo ya HELB kwa wanafunzi wa vyuo vya kibinafsi

Tom Mathinji

Mahakama iko tayari kwa kesi za uchaguzi mkuu ujao asema Jaji mkuu Martha Koome

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi