Wanariadha wa Kenya watafungua msimu wa Diamond league Ijumaa usiku katika mkondo wa kwanza wa Doha Qatar.
Bingwa wa dunia katika mita 1500 Timothy Cheruiyot atapambana na bingwa wa Kip Keino Classic mwaka huu Abel Kipsang,Timothy Sein ,Charles Simotwo na Etiang’ Kamar ,huku wakipata ukinzani kutoka kwa Waethioipia wakiongoza na mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 10,000 Yomif Kejelcha ,Lemmi Tedese na Samuel Zeleke .
Bingwa wa Olimpiki katika mita 1500 Faith Kipyegon atajitosa katika mita 3000 pamoja na bingwa wa dunia katika mita 3000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech na Beatrice Chebet na Ednah Jebitok.
Wakenya hao watapambana na Winnie Nanyondo kutoka Uganda na Waethiopia Fantu Worku ,Melkat Wodu,Fantaye Belayneh,GEBRZIHAIR Girmawit,WELDE Bertukan,ABEBE Mekides
na Francine Niyonsaba kutoka Burundi.
Mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki Ferguson Cheruiyot atatimka fainali ya mita 800 pamoja bingwa wa dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Noah Kibet ,wakipimana nguvu na Donovan Brazier wa USA na Marco Arop wa Canada.
Mshindi wa nishani ya shaba ya olimpiki Bejamin Kigen atatimka mita 3000 kuruka viunzi na maji pamoja na Leonard Bett,Lawrence Kemboi na Abraham Kibiwott huku wakipata ukinzani mkali kutoka kwa bingwa wa Olimpiki Soufiane El Bakalli wa Moroko na Lamecha Girma wa Ethiopia .

Mashindano ya Diamond league hushirikisha mikondo 14 ambayo huandaliwa katika miji mbalimbali.