Wakenya kujitosa Uingereza kwa mkondo wa kwanza wa Diamond league wa Gateshead

Mkondo wa kwanza wa mashindano ya Diamond league utaandaliwa  Jumapili hii terehe 23 Mei ,nchini Uingereza   ukijulikana kama  Gateshead ,huku Wakenya wakijitosa uwanjani katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji ,mita 1500 na mita 5000.

Mshindi wa nishani ya fedha ya mita 3000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji  katika michezo ya jumuiya ya madola  mwaka 2018 ,Abraham Kibiwott ,mshindi wa nishani ya fedha ya dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 katika mta 3000 kuruka maji na viunzi   mwaka 2018 Leonard Bett watajitosa uwanjani katika  shindano hilo la kufungua msimu wa Diamond league.

Also Read
Cherono ataka Athletics Kenya kuwateua makocha wa Kike kuwasimamia wasichana

Upinzani kwa Wakenya utatoka kwa Hilary Bor na Stanley Kebenei  wa Marekani na  mshindi wa nishani ya shaba ya dunia mwaka 2017 Sofiane El Bakkali wa Moroko.

Bremin Kiprono ndiye Mkenya pekee atakayetimka mita 1500 akipambana na bingwa wa ulaya Jakob Ingebrigsten wa Norway na Ronald Musagala wa Uganda.

Bingwa wa dunia katika mita 10,000 mwaka 2017 Nicholas Kimeli  Kipkorir atapambana na Jacob Krop na  Michael  Kibet .

Shindano jingine linalotarajiwa kusisimua ni mita 100 wanawake itakayowakutanisha bingwa mara mbili wa Olimpiki Shelly Ann Freyser Pryce wa Jamaica,bingwa dunia Din Asher Smith,bingwa mara mbili ya jumuiya ya madola Blessing Okagbare wa Nigeria ,mshindi nishani ya fedha mara mbili katika mashindano ya dunia na bingwa wa bara Amerika kwa chipukizi Shar Carri Richardson wa Marekani .

Also Read
Empoli FC yarejea ligi kuu Italia Serie A baada ya misimu miwili

Mkondo huo wa Uingereza utafuatwa na ule wa Doha Qatar Mei 28 na ule wa Italia Juni 10.

Mikondo mingine ya diamond league itakayoandaliwa kabla ya michezo ya Olimpiki ni ile ya Olso Julai mosi ,Stockholm Julai 4 ikifuatwa na ile ya Monaco na London Julai 9 na 13 mtawalia.

Ratiba ya Diamond League mwaka 2021

 

28 MAY 2021 Diamond League Meeting Suhaim bin Hamad Stadium, Doha QATAR
10 JUN 2021 Golden Gala Pietro Mennea Stadio Luigi Ridolfi, Firenze ITALY
01 JUL 2021 Bislett Games Bislett Stadion, Oslo NORWAY
04 JUL 2021 Bauhaus-Galan Olympiastadion, Stockholm SWEDEN
09 JUL 2021 Herculis EBS Stade Louis II, Monaco MONACO
13 JUL 2021 Müller Anniversary Games Olympic Stadium, London GREAT BRITAIN & N.I.
14 AUG 2021 Diamond League Meeting Shanghai Stadium, Shanghai PR OF CHINA
21 AUG 2021 Prefontaine Classic Hayward Field, Eugene, OR UNITED STATES
22 AUG 2021 China 2 DL TBC
26 AUG 2021 Athletissima Stade Olympique de la Pontaise, Lausanne SWITZERLAND
28 AUG 2021 Meeting de Paris Stade Charléty, Paris FRANCE
03 SEP 2021 Allianz Memorial Van Damme Boudewijnstadion, Bruxelles BELGIUM
08 SEP 2021 – 09 SEP 2021 Weltklasse Letzigrund, Zürich
  

Latest posts

Wabunge wa Kenya wawakwatua Wabunge wa Tanzania mabao 3-1

Dismas Otuke

Senegal timu ya kwanza ya Afrika kushinda mechi ya Kombe la Dunia Qatar

Dismas Otuke

Betika,yapeleka kundi la kwanza la mashabiki 60 Qatar kufurahia kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi