Wakenya wahimizwa kujiunga na Taasisi za kiufundi kuboresha ukuaji wa viwanda nchini

Kamishna wa kaunti ya Machakos John Ondengo ametoa wito kwa wadau wa elimu hapa nchini kuwahamasisha wakenya kuhusu manufaa ya taasisi za mafunzo ya kiufundi almaarufu TVETs.

Akizungumza katika mkutano wa kamati shirikishi ya utekelezaji wa maendeleo ya kaunti, Ondengo alidokeza kuwa idadi ya wanaojiunga na vyuo anuwai ingali ni ya chini kutokana na ukosefu wa habari kwani wengi wana dhana kuwa taasisi hizo ni za wale ambao walianguka mtihani au walioacha shule.

Taasisi za TVETs hutekeleza wajibu mkubwa katika ukuaji wa viwanda na wakuu wa vitengo wanapaswa kuhakikisha idadi ya wanaojiunga na taasisi hizo inaongezeka,” alisema kamishna huyo wa kaunti.

Kamishna huyo wa kaunti alipongeza taasisi ya kiufundi ya Machakos kwa wasio na uwezo wa kuona kwa kuwapa wanafunzi hao ujuzi wanaohitaji hasaa ushonaji wa viatu.

Hata hivyo Ondego alidokeza kuwa baadhi ya changamoto zinazokumba taasisi za kifundi nchini ni pamoja na miradi iliyokwama huku akitoa wito kwa idara ya ujenzi kukamilisha miradi yote iliyokwama.

Kwa upande wake naibu mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Machakos Simon Mutemi, alisema wizara ya elimu imejitolea kupiga jeki taasisi za kiufundi kuhakikisha zinatimiza kikamilifu malengo yao.

Kaunti ya Machakos ina taasisi tatu za kiufundi ambazo zinaendeshwa na serikali ya kitaifa, ambazo ni Taasisi ya kiufundi kwa wasio na uwezo ya kuona, Taasisi ya kiufundi ya Katine na Taasisi ya kiufundi ya Masinga.

Serikali ya kitaifa iko katika harakati za kujenga taasisi mbili zaidi za kiufundi ambazo zitakuwa Machakos mjini na katika kaunti ndogo ya Yatta.

  

Latest posts

Rais Kenyatta amwomboleza Nancy Karoney, dadake waziri wa ardhi Farida Karoney

Tom Mathinji

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi