Wakenya wahimizwa kurejelea shughuli zao za kila siku

Siku moja baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura za Urais,  mkuu wa utumishi wa umma aliyepia mwenyekiti wa kamati ya kitaifa kuhusu usalama NSAC Joseph Kinyua, ametoa wito kwa wakenya kurejelea shughuli zao za kila siku.

Akizungumza baada baada ya mkutano wa kamati ya usalama siku ya Jumanne, Kinyua aliwahakikishia kuwa serikali inaendelea na itaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha taifa hili ni salama.

Also Read
Somalia yafungua tena ubalozi wake Jijini Nairobi

“Kamati ya kitaifa ya usalama ingependa kuwahakikishia wakenya wote na raia wengine walio humu nchini kwamba serikali imechukua hatua zote kuweka usalama hapa nchini. Ninatoa wito kwa wakenya na jamii ya wanabiashara kurejelea shughuli zao za kila siku katika ujenzi wa taifa hili,”alisema Kinyua.

Also Read
Ni wageni 5,000 watakaohudhuria sherehe za Jamuhuri katika uwanja wa Nyayo

Kinyua pia alipongeza huduma ya taifa ya polisi na asasi zingine za usalama kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa kipindi cha uchaguzi Mkuu.

Also Read
Yafahamu haya kuhusu chanjo ya AstraZeneca

Aidha mkuu huyo wa utumishi wa umma, alisema kutangazwa kwa matokeo ya kura za Urais, kumeanzisha mchakato wa kikatiba wa mpito wa serikali.

  

Latest posts

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

NHIF yaongeza muda wa kuwapa bima ya afya maafisa wa Polisi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi