Wakenya wajiunga na jamii ya Waislamu kuadhimisha Eid al-Adha

Wakenya wamejiunga na jamii ya waislamu kuadhimisha sherehe za Eid al-Adha, ambazo ni miongoni mwa sherehe mbili za kiislamu.

Eid al-Adha, ambalo ni jina la kiarabu linalomaanisha sherehe ya dhabihu, huashiria jinsi Abrahamu alivyotii agizo la mwenyezi Mungu la kumtoa mwana wake wa pekee Isaka kama dhabihu.

Viongozi wa kisiasa, mashirika pamoja na wasamaria wema walituma jumbe za heri njema kwa jamii ya Waislamu wanapoadhimisha siku kuu ya Eid al-Adha.

Also Read
Mtu mmoja auawa na mwili wake kutupwa kando ya barabara Transmara

Naibu wa Rais Dkt William Ruto kupitia kwa akaunti yake ya twitter aliwatakia Waislamu heri njema wakati wa sherehe hizi huku akitaka siku hii kuwapa motisha wakenya kufanya kazi kwa manufaa ya kila mmoja.

Siku ya Jumatatu Ruto aliwapatia mbuzi jamii ya waislamu katika kaunti ya Mombasa kabla ya sherehe hizo.

Also Read
Rais Kenyatta: Ushirikiano thabiti wa kimataifa ni nguzo muhimu kukabiliana na changamoto zilizopo

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, naye pia aliwatumia ujumbe wa heri njema akiwatakia baraka za mwenyezi Mungu. Aliwataka waislamu kuwa imara katika imani yao.

Naye kiongozi wa  ANC Party Musalia Mudavadi kwa upande wake aliitakia jamii ya waislamu amani na furaha wanapoadhimisha siku kuu ya Eid al-Adha.

“Huu ni wakati wa kutafakari dhabihu nyingi ambazo tumetoa kwa maendeleo ya taifa hili. Mnapo adhimisha sherehe hizi mwenyezi Mungu apokee dhabihu zenu,” alisema Mudavadi.

Also Read
Mashirika yanayokabiliana na mihadarati yatakiwa kuimarisha vita dhidi ya uraibu huo

Kiongozi wa wiper Kalonzo Musyoka naye pia aliwatakia waislamu wote amani, furaha na mafanikio wakati wa maadhimisho ya Eid al-Adha.

Wakati wa maadhimisho ya sherehe za Eid al-Adha, wanyama hutolewa kama dhabifu ambapo robo tatu ya wanyama hao huliwa na familia na robo iliyosalia hupatiwa wasiojiweza katika jamii.

  

Latest posts

Aden Duale: Uchaguzi Mkuu sharti uandaliwe tarehe 9 mwezi Agosti mwaka 2022

Tom Mathinji

Mudavadi asema taifa hili halipaswi kushuhudia ghasia kama zile za mwaka 2007

Tom Mathinji

Malkia Strikers wajizatiti lakini waanguka seti 3-0 mikononi mwa wenyeji Japan

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi