Wakenya walenga kulipiza cha Olimpiki katika mita 3000 kuruka viunzi na maji katika Kip Keino Classic

Wakenya 8 watajitosa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani Jumamosi jioni kwenye makala ya pili ya mashindano ya Kip Keino Classic wakilenga kulipiza kisasi cha kupoteza taji ya Olimpiki ya mita 3000 kuruka viunzi na maji kwa mara ya kwanza mwezi uliopita mjini Tokyo Japan,Soufiane El Bakkali wa Moroko akiwatesa wakati huo.

Hata hivyo Wakenya hao wanaowajumuisha chipukizi na wanariadha waliokubuhu watashuka katika uwanja wa Kasarani kuanzia saa kumi na moja na dakika 32 jioni kumenyana na Bakkali aliyeshinda dhahabu ya Olimpiki .

Also Read
Mali yatinga nusu fainali ya CHAN baada ya kuilaza Congo 5-4

Kikosi cha Kenya kinawajumuisha bingwa wa dunia katika mbio hizo kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Amos Serem anayerejea uwanjani Kasarani chini ya mwezi mmoja tangu atwae dhahabu ya dunia ,Nicholas Bett aliyeshinda nishani ya fedha ya dunia katika mbio za mita 2000 kuruka viunzi na maji kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 ,mwaka 2013,bingwa wa dunia katika mita 2000 kuruka maji na viunzi kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 mwaka 2017 leonard Bett.

Also Read
Bingwa wa dunia Timothy Cheruiyot kuwika Kip Keino Classic Jumamosi

Washiiriki wengine wa Kenya katika shindano hilo ni Wilberforce KOnes,Amos Kirui,Vincent Kichupmba pamoja na mshindi wa nishani ya shaba ya olimpiki mwaka huu Benjamin Kigen na watapambana na El Bakkali,Hilal Yergo wa Uturuki na Samuel Firehu wa Ethiopia.

Also Read
Obiri kuwatumbuiza mashabiki Kip Keino Classic

Mbio za akina dada pia zitashuhudia mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki mwaka huu Hyvin Kiyeng akiwaongoza wenzake Mercy Chepkurui,Purity Kirui,Celphine Chespol,Jackline Chepkoech wakitoana jasho na winred Mutile Yavi wa Bahrain,bingwa wa Olimpiki Peruth Chemutai wa Uganda,Lomi Muleta wa Ethiopia na Daizy Chepkemoi wa Kazakistan.

(From L) Ethiopia’s Samuel Tefera, Kenya’s Timothy Cheruiyot, Australia’s Oliver Hoare and France’s Alexis Miellet compete in the men’s 1500m heats during the Tokyo 2020 Olympic Games at the Olympic Stadium in Tokyo on August 3, 2021. (Photo by Giuseppe CACACE / AFP) (Photo by GIUSEPPE CACACE/AFP via Getty Images)
  

Latest posts

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Ni Siku ya Ndovu kumla mwanawe Tusker dhidi ya Zamalek Nyayo

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi