Wakenya Waonekana Kuchangamkia Uongozi wa Wanawake

Kwa muda mrefu wanaume nchini Kenya waling’aa kwenye nyadhifa za kuchaguliwa huku kukiwa na wanawake wachache mno hadi mwaka 2010 wakati katiba mpya ya Kenya kuagiza kwamba thuluthi moja ya nyadhifa za uongozi zitengewe watu wa jinsia moja ambayo kwa wakati huo ililenga kina mama. Ili kusaidia kuafikia hitaji hilo, kulibuniwa wadhifa wa mwakilishi wa kike wa kaunti bungeni huku wengine wachache wakichaguliwa kwenye nyadhifa za kumenyana na wanaume.

Uchaguzi wa mwaka 2022 umeleta taswira tofauti ambapo kina mama wengi wameingia kwenye nyadhifa za juu kama vile ugavana na useneta. Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Mumbi Waiguru amehifadhi wadhifa huo ambao alishinda mara ya kwanza kupitia chama cha Jubilee na sasa amerejea kupitia chama cha UDA. Mshindani wake wa karibu alikuwa mwanamke Bi. Purity Wangoi Ngirici.

Also Read
COVID-19: Kenya yanakili visa vipya 495 huku wagonjwa 19 wakifariki

Katika kaunti ya Machakos Bi. Wavinya Ndeti wa chama cha Wiper alitangazwa mshindi wa wadhifa wa ugavana ambao amewania mara mbili awali. Nelly Illongo msimamizi wa uchaguzi katika kaunti hiyo alimtangaza Wavinya Ijumaa alfajiri katika kituo cha kujumlisha kura cha Machakos Academy. Wadhifa wa useneta katika kaunti hiyo umeendea Agnes Kavindu wa chama cha Wiper pia wadhifa ambao ameshikilia tangu mwaka 2021 kufuatia kifo cha seneta Boniface Kabaka Disemba mwaka 2020.

Also Read
Mwaniaji Urais wa Muungano wa Azimio Ahudhuria Ibada

Kaunti ya Nakuru pia imeteua kina mama katika nyadhifa za ugavana, useneta na ubunge. Susan Kihika ndiye gavana na seneta ni mfanyibiashara Tabitha Karanja. Liza Chelule amehifadhi wadhifa wa mwakilishi wa kike wa kaunti bungeni huku Martha Wangare, Irene Njoki, Jane Kihara na Charity Kathambi wakichaguliwa wabunge wa maeneo ya Gilgil, Bahati, Naivasha na Njoro mtawalia. Yapo maeneo bunge katika kaunti hiyo ya Nakuru ambayo yanaongozwa na wanaume pia.

Also Read
Baadhi ya maeneo Jijini Nairobi yakumbwa na ukosefu wa nguvu za umeme

Fatuma Achani ndiye gavana wa kaunti ya Kwale, Kawira Mwangaza kaunti ya Meru, Gladys Wanga Homa Bay na Cecily Mbarire katika kaunti ya Embu. Hatua ya Kenya ya kubadili nia kuhusu uongozi wa wanawake utasaidia sana katika kutekeleza hitaji la katiba la thuluthi moja ya viongozi wawe wa jinsia moja na kuondolea mbali hatari ya nyumba za uongozi kuvunjwa kupitia agizo la mahakama.

  

Latest posts

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

NHIF yaongeza muda wa kuwapa bima ya afya maafisa wa Polisi

Tom Mathinji

Moses Kuria avunja chama chake na kujiunga na UDA

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi