Wakenya watahadharishwa dhidi ya kula nyama zisizokaguliwa msimu huu wa sherehe

Huku Wakenya kote nchini wakiendelea na tafrija za msimu wa sherehe, ipo hofu ya ongezeko la biashara ya nyama ambayo haijakaguliwa, ambayo huenda ikahatarisha maisha ya walaji.

Chama cha wataalam wa ukaguzi wa nyama Barani Afrika kimeonya kwamba wafanyabiashara walaghai wanatumia fursa ya kuwepo kwa wateja wengi wa nyama katika Kaunti ya Kajiado na sehemu nyingine za humu nchini kuchinja mifugo usiku.

Also Read
Wakazi wa Narok wahimizwa kuchukua vitambulisho vyao kwenye Kituo cha Huduma

Rais wa chama hicho Benson Oduor Omeda amesema uchunguzi wao umebaini kuwa nyama nyingi ambazo hazijakaguliwa zinauzwa, huku nyingine zikipikwa kwenye migahawa ya humu nchini.

Also Read
Wanyakuzi wa ardhi ya umma waagizwa kuirejesha kwa miradi ya maendeleo

Chama hicho kimeongeza kuwa huku vichinjio vikimilikiwa na watu binafsi, usafirishaji nyama kutothibitiwa na ukaguzi wa nyama kugatuliwa, usalama wa nyama hauzingatiwi ipasavyo.

Also Read
Viongozi wa Kilifi waibua wasi wasi kutokana na ongezeko la visa vya COVID-19

“Hii inawapa nafasi watu wengine kuchinja mifugo mahali popote, nyumbani kwao au msituni kisha wasafirishe nyama hizo hadi kwa vichinjio,” ameonya Omeda.

Chama hicho kimewashauri wakenya kuwa waangalifu kuhusu nyama wanayoila.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi