Wakenya watahadharishwa dhidi ya kulegeza masharti ya kudhibiti Covid-19

Katibu katika wizara ya afya Susan Mochache,amewataka wakenya kuendelea kuzingatia maagizo ya kuzuia msambao wa virusi vya Corona na kuchanjwa katika juhudi za kuepukana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Dkt. Mochache alisema wanasayansi wameonya kuwa aina mpya ya virusi vya ugonjwa huo yenye makali kuliko aina ya virusi vya corona vya Delta na Omicron, huenda vikachipuka, huku akikariri umuhimu wa kuchanjwa,kutumia barakoa na kuepukana na maeneo ya watu wengi katika juhudi za kukabiliana maambukizi hayo.

Also Read
EU kudhibiti uuzaji wa chanjo za kukabiliana na Covid-19

Katibu huyo alisema hayo akiwa Baricho kaunti ndogo ya Malindi, Kilifi ambapo makatibu tisa walizuru mradi wa ujenzi wa barabara kati ya Marikebuni, Marafa na Sosoni unaotekelezwa na serikali ya kitaifa kwa gharama ya shilingi bilioni nne.

Also Read
Washukiwa wawili wakamatwa kwa kuwawekea watu dawa katika vinywaji kabla kuwaibia

Mochache alisema waliochanjwa wanaweza kustahimili makali ya ugonjwa huo.,

Hayo yanajiri huku watu wengine 1,175 wakiambukizwa ugonjwa wa Covid 19 hapa nchini baada ya sampuli 10,073 kupimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi ya Covid-19 hapa nchini sasa ni cha  asilimia 11.7.

Mhasiriwa wa umri wa chini ni mtoto wa umri wa  miaka miwili huku wa umri wa juu akiwa na umri wa miaka 108.

Also Read
Kenya yanakili visa 170 vipya vya COVID-19

Jumla ya visa 315,665 vya maambukizi vimenakiliwa nchini baada ya sampuli 3,127,480.

Wagonjwa wengine 3,025 wamepona ugonjwa huo na kuongeza idadi ya waliopona kutimia 279,044.

Wagonjwa  watatu zaidi wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo na kuongeza idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo hadi 5,472.

  

Latest posts

Washukiwa wawili wakamatwa na pembe za ndovu kaunti ya Busia

Tom Mathinji

Shujaa yaipakata Canada alama 24-5 katika msururu wa Seville Uhispania na kufufua matumini ya kutinga robo fainali

Dismas Otuke

Serikali ya Mombasa yalaumiwa kwa kushindwa kufunga jaa la taka la VOK

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi