Wakili wa Sonko kwenye kesi ya ufisadi ajiondoa

Wakili mkuu wa aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko kwenye kesi ya ufisadi inayohusisha shilingi milioni 10, John Khaminwa amejiondoa kwenye kesi hiyo.

Khaminwa ameondoka mahakamani akidai kulikuwa na upendeleo na kwamba upande wa mashtaka haujakabidhi upande wa utetezi stakabadhi zinahiotajika katika kesi hiyo.

Aidha amedai kwamba Hakimu Mkuu wa mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi Douglas Ogoti ameonyesha upendeleo wazi wazi kwa kutokubali ushauri wa daktari unaomtaka Sonko apumzike.

Khaminwa amesema kundi lake linahitaji muda zaidi ili kukusanya ushahidi wa kutosha kumtetea mteja wake.

Also Read
Kibicho ajisalimisha kwa DCI baada ya Sonko kumhusisha na vitendo vya uhuni
Also Read
Kenya huenda ikapoteza shilingi bilioni 360 kupitia miradi ambayo haijakamilika

Amehoji kuwa uamuzi wa mahakama wa kuzuia vyombo vya habari kuhudhuria vikao vya kesi hiyo ni kinyume cha sheria, akidai kwamba mteja wake hatatendewa haki.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi