Wakimbizi wa Afghanistan wawasili Uganda

Kundi la kwanza la watu 51 waliohamishwa kutoka nchini Afghanistan limewasili nchini Uganda.

Kundi hilo liliwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebbe kupitia ndege iliyokodishwa.

Serikali ya Uganda imesema kundi hilo linapitia nchini Uganda kabla ya kuelekea mataifa mengine ikiwemo Marekani.

“Serikali ya Uganda Jumatano asubuhi ilipokea watu 51 waliohamishwa kutoka Afghanistan, waliwasili na ndege iliyokodishwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe,” ilisema taarifa ya wizara ya mashauri ya kigeni ya Uganda.

Also Read
Majirani wa Afghanistan watakiwa kuacha wazi mipaka yao

Haijabainika wazi ni kwa muda gani watahifadhiwa nchini Uganda. Watu hao waliohamishwa wanajumuisha wanaume,wanawake na watoto ambao tayari wamepimwa kuthibitisha kama wana ugonjwa wa Covid-19 au la na watawekwa karantini kwa mujibu wa taarifu iliyotolewa.

Also Read
Zari Akanusha Madai Ya Kutambulisha Mpenzi

Uhamisho huo unafuatia ombi la serikali ya America kwa Uganda kuwahifadhi watu waliotoroka Afghanistan kutokana na ghasia zinazoshuhudiwa huko tangu kundi la Taliban kuchukua uongozi.

Taifa la Uganda linahifadhi zaidi ya watoro milioni moja waliotoroka nchini mwao kutokana na mizozo mbalimbali kote katika mataifa yaliyoko kwenye kanda ya Afrika Mashariki.

Also Read
Asilimia 90 ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wafika shuleni

Marekani inajizatiti kuhakikisha inakamilisha shughuli za kuwahamisha watu pamoja na kuwaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan ifikapo mwisho wa mwezi Agosti huku Kundi la Taliban likidinda kuongeza muda huo.

Na BBC

  

Latest posts

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi