Walimu watakiwa kuwa mfano bora katika ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili

Huku lugha ya kiswahili inapozidi kupata nafasi katika mataifa ya Afrika hususan kwa kuorodheshwa kuwa miongoni mwa lugha ya taifa, walimu wa lugha ya Kiswahili hapa nchini wamehimizwa kuwa mfano mwema na kuwachochea wanafunzi kukumbatia na kuipenda lugha ya kiswahili.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Oxford University Press kanda ya Afrika Mashariki John Mwazemba, baadhi ya walimu huzungumza Kiswahili sanifu wakiwa darasani tu, lakini punde somo la kiswahili linapofika mwisho, wao hawazungumzi tena Kiswahili.

Also Read
Akina mama na watoto wenye akili taahira wapokea msaada wa vyakula na mavazi kutoka Women Empowerment Kenya

Mwazemba alisema hali hiyo inakosa kuwapa wanafunzi motisha ya kukipenda kiswahili hivyo basi kuhujumu ukuaji wa lugha hiyo.

Akizungumza Jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa toleo la nne la Kamusi ya Kiswahili sanifu, Mwazemba alidokeza kuwa Lugha ya Kswahili inakua kwa kasi sana kwani lugha hii hubadilika kila baada ya miaka mitano.

Uzinduzi wa Toleo la nne la Kamusi ya Kiswahili Sanifu. (Picha na Selestus Mayira)

Kulingana naye ni kutokana na mabadiliko hayo ndiposa Oxford University Press baada ya utafiti wa kina, iliazimia kuchapisha toleo hilo la nne la Kamusi ya Kiswahili kama njia mojawepo ya kuhakikisha wasomaji wanayafahamu maneno mapya.

Also Read
Ukusanyaji saini za BBI kuanza rasmi leo

Mkurugenzi huyo aliisifu lugha ya Kiswahili, akisema imetekeleza jukumu muhimu la kuimarisha utangamano sio tu humu nchini bali pia Afrika Mashariki na kanda nzima kwa jumla.

Kamusi hiyo mpya iliyozinduliwa ina maneno 1,000 mapya yaliyojumuishwa na pia imeelezea jinsi ya kuyatamka. Kulingana na Mwazemba Toleo hili jipya limerahisisha utumizi wa Kamusi.

Katiba ya Kenya ya mwaka wa 2010 inaelezea kuwa Kiswahili na Kingereza ni lugha rasmi na pia za taifa. Hivi majuzi bunge la taifa lilizindua kanuni za bunge zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Also Read
Helikopta ya Kijeshi yaanguka Kajiado

Licha ya kuwa Kiswahili ni lugha rasmi nchini Tanzania na Kenya, nchi zingine za Afrika Mashariki kama vile Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kiswahili ni lugha ya taifa. Mataifa mengine yanayozungumza Kiswahili ni pamoja na  Burundi, Msumbiji, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Zambia.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi