Walinitishia maisha! Van Vicker

Muigizaji mzaliwa wa nchi ya Ghana Van Vicker amefunguka kuhusu ushindani ulioko katika sekta ya filamu nchini Nigeria almaarufu Nollywood.

Wengi walipata kumfahamu Vicker kutokana na filamu alizoigiza za Nigeria wasijue yeye ni mzaliwa wa Ghana na sio Nigeria.

Akizungumza maajuzi katika kipindi kimoja cha mahojiano nchini Ghana, Vicker alifichua kwamba kuna wakati waigizaji nyota wa kiume nchini Nigeria walimtishia maisha.

Also Read

Kisa na maana alikuwa anapata kazi nyingi za uigizaji nchini Nigeria na kuwa mhusika mkuu jambo ambalo hawakufurahia.

“Unajua mtayarishaji filamu akikuangazia inakuwa kwamba ni wewe tu kila mara. Na ikiwa ni wewe basi yule mwingine anakosa.” Alisema Van.

Joseph Van Vicker alizaliwa tarehe mosi mwezi Agosti mwaka 1977, mamake ana asili ya Ghana na Liberia na babake ni mjerumani na aliaga dunia Van akiwa na umri wa miaka sita tu. Van ana mke kwa jina “Adjoa” na walifunga ndoa mwaka 2003 na wana watoto watatu.

Also Read
Ushauri wa Professor Jay

Anampenda sana mamake na kwake yeye ndiye shujaa wa maisha yake. Alianza na utangazaji katika vituo mbali mbali vya redio nchini Ghana kabla ya kuingilia utangazaji wa Televisheni na baadaye uigizaji.

Also Read
Tanasha Donna aandaa tamasha

Muigizaji huyo hakutaja majina ya waigizaji maarufu wa Nigeria ambao walimtishia maisha kwa kuchukua nafasi zao za kazi.

Mwaka 2014 Van Vicker aliigiza kwenye filamu kwa jina ‘Day After Death’ na muigizaji wa nchi ya Tanzania Wema Sepetu.

Wema Sepetu na Van Vicker
  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi