Waliokuwa madiwani walalamika kutelekezwa na Serikali ya Kitaifa

Waliokuwa madiwani wakati wa serikali za mitaa katika kaunti ya Bungoma wameelezea kutelekezwa  na serikali ya kitaifa licha ya kuwa walifanya mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa hili.

Kwa sasa madiwani hao wamesema wanazidi kuishi katika hali ya ufukara huku wakidai kuwa hawapati msaada kutoka kwa serikali kuu.

Madiwani hao wa zamani wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kuingilia kati na  kuwatetea ili wapate fedha sawia na viongozi waliojitolea kikazi katika eneo hilo kabla ya ugatuzi.

Also Read
Baraza awarai wakaazi wa Bungoma kujiandikisha kwa wingi kupiga kura

Katika mazungumzo na wanahabari, mwenyekiti wa madiwani hao kaunti ya Bungoma, Augustine Tela, alisena kuwa wakati wa hatamu zao walikuwa wakipata malipo duni kinyume na wawakilishi wadi wa sasa wanaopata mshahara wa kumezewa mate.

Also Read
Soko la Gikomba lateketea tena

Kwa mujibu wa Tela madiwani hao wanapitia magumu kwa kukosa pesa za kukithi mahitaji ya  familia zao.

Tela alitoa wito kwa Gavana Wycliffe Wangamati kuingilia kati na kuona kuwa  maslahi ya madiwani hao  wa zamani yanashughulikiwa kikamilifu.

Hata hivyo akizungumza wakati wa mkutano ulioandaliwa katika eneo la saint Patrick pastoral centre, wadi ya Kabula kwenye eneo bunge la Bumula, uliowaleta pamoja  madiwani wa zamani wapatao 265 kutoka maeneo bunge yote ya kaunti, Gavana wa Bungoma Wycliffe  Wangamati aliwaahidi kuwa tayari mikakati kabambe imewekwa ili kuhakikisha kuwa wanastawishwa kikamilifu.

Also Read
Didmus Barasa Kufikishwa Mahakamani Leo

Aidha Wangamati alitumia fursa hiyo kuwashawishi viongozi hao japo waling’atuka mamlakani kumuunga mkono katika juhudi zake za kuimarisha maendeleo katika kaunti hii.

 

 

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Majukumu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua yabainishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi