Waliotekeleza ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/2008 mashakani

Waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/2008, waliandikisha upya taarifa katika makao makuu ya idara ya upelelezi wa jinai Jijini Nairobi.

Jumla ya visa 72 vya mauaji, 44 vya watu kuachwa bila makazi na vitisho 118 vilinakiliwa kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi huo kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti.

Also Read
William Ruto amtakia Raila Odinga afueni ya haraka

Akiwahutubia waathiriwa hao wa ghasia za baada ya uchaguzi katika makao makuu ya idara ya upelelezi wa jinai jijini Nairobi, Kinoti aliwahakikishia waathiriwa kwamba watafuatilia yote walionakili Jumatatu kuhusiana na ghasia hizo za baada ya uchaguzi mwaka wa 2007 na 2008.

Also Read
Rigathi Gachagua kusalia korokoroni mwishoni mwa juma

Mkurugenzi huyo wa idara ya upelelezi alisema serikali imeagiza ofisi yake kuhakikisha kwamba hakuna ghasia zaidi wala vifo zinvyoajiri humu nchini.

Kinoti alihakikishia umma kwamba waliotekeleza ghasia hizo watashtakiwa humu nchini mara uchunguzi utakapokamilika.

Also Read
Muungano wa upinzani wa NASA wasambaratika

Waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi walianza kuandikisha taarifa Jumapili katika makao makuu ya idara ya upelelezi.

Ghasia zilizuka baada ya aliyekuwa rais wa taifa hili Mwai kibaki kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliokumbwa na ushindani mkali.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi