Walishaji mifugo waliovamia mashamba ya wenyewe wapewa makataa ya kuondoka

Serikali imewapa walishaji mifugo ambao wamevamia mashamba makubwa ya kibinafsi ya ufugaji katika kaunti ya Laikipia makataa ya siku saba kuondoka la sivyo waondolewe kwa nguvu.

Waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiang’i, aliyezuru kaunti hiyo alisema serikali haitazama huku walishaji mifugo wakivamia mashamba ya kibinafsi ya ufugaji na kusababisha ukosefu wa usalama katika sehemu hiyo.

Also Read
Waathiriwa 300 wa mkasa wa moto Kangemi wapata msaada kutoka kwa Ananda Marga Mission

Waziri ambaye alikuwa akiongea katika KambiĀ  ya maafisa wa kukabiliana na wizi wa mifugo ya Naibor iliyoko kaunti ndogo ya Laikipia kaskazini, alisema kikosi maalum cha maafisa wa polisi na jeshi la ulinzi la Kenya ,kitapelekwa katika hifadhi ya Kirimon ili kuwazuia walishaji mifugo kuvuka kutoka kaunti za Isiolo na Samburu.

Also Read
Maafisa wa polisi waonywa dhidi ya utovu wa nidhamu

Waziri Matiang’i alisema serikali ya kitaifa itashirikiana na serikali za kaunti kwenye mpango ambapo watauzia mifugo shirika la Kenya Meat Commission, ili waweze kupunguza idadi ya mifugo wao wakati huu wa kiangazi na kuongeza idadi hizo wakati hali ya anga itakapoimarika.

Also Read
Wakenya kuanza kupokea Huduma Namba Desemba

Aliwaonya wanasiasa dhidi ya kuchochea ghasia wakati huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia.

  

Latest posts

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi