Wanafunzi 10 wanaofanya mtihani wa KCSE wajifungua eneo la Bomet Mashariki

Watahiniwa kumi wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE katika kaunti ndogo ya Bomet Mashariki wanafanyia mtihani huo katika hospitali mbali mbali baada ya kujifungua jana.

Maafisa wa elimu katika kaunti ya Bomet wamesema watahiniwa kutoka shule saba za kaunti hiyo ndogo wako katika hali dhabiti na wameweza kufanya mitihani yao wakiwa kwenye wadi za kujifungulia kina mama bila tatizo lolote.

Kwingineko katibu mwandamizi wa wizara ya mafuta na uchimbaji madini mhandisi John Mosonik ameelezea wasi wasi kutokana na visa vya mimba miongoni mwa watahiniwa wa mtihani wa KCSE katika kaunti ndogo ya Bomet Mashariki .

Mosonik ametoa wito kwa viongozi na maafisa wa utawala kukabiliana na wale wanaotunga mimba wanafunzi.

Mosonik ambaye alikuwa akiongea katika shule ya upili ya Mulot alipokamilisha shughuli ya kusimamia mitihani kwa muda wa siku nne katika kaunti ya Bomet, alisema ni dhahiri shahiri kuwa hali ya wanafunzi kurundika ndiyo iliyokuwa changamoto katika shule nyingi na kutoa wito kwa wazazi kuwekeza katika muundo msigi wa shule.

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi