Wanafunzi 12 wakamatwa kwa kuteketeza bweni katika shule ya upili ya Mukaa

Shule ya upili ya Mukaa Boys imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya bweni moja kuteketezwa kwa moto siku ya Jumamosi kufuatia mgomo wa wanafunzi. 

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ndogo, Beatrice Makau, alithibitisha kwamba zaidi ya wanafunzi 1,260 wali-amriwa kwenda nyumbani siku ya Jumatatu ili kutoa nafasi ya kufanya uchunguzi kuhusu kisa hicho ambapo mali yenye thamani isiyojulikana iliharibiwa. 

Hadi sasa wanafunzi 12 wametiwa nguvuni kwa madai ya kujihusisha kwao na uteketezaji huo wa bweni la zaidi ya wanafunzi 200.

Makau alisema uamuzi wa kuwapeleka nyumbani wanafunzi hao uliafikiwa ili kutuliza wasi wasi uanozidi kuongezeka, kuchunguza kisa hicho na pia kufanya ukarabati. 

Kulingana na kamanda wa polisi katika kaunti hiyo, Joseph Ole Naipeyan, wanafunzi walianzisha mgomo wao mwendo wa saa kumi na mbili jioni siku ya Jumamosi na kuteketeza bweni.

Kamanda huyo wa polisi aliongeza kwamba jaribio jingine la kuteketeza bweni lilizimwa saa kumi na mbili unusu jioni siku ya Jumapili.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi