Wanafunzi 5,000 ambao shule zao ziliathiriwa na mafuriko wahamishwa

Zaidi ya wanafunzi 5,000 kutoka jumla ya shule-16 zilizofurika maji kutoka maziwa ya Baringo na Bogoria, wamehamishiwa kwenye taasisi nyingie ili kuhakikisha hawapotezi masomo wakati huu ambapo shule zimefunguliwa upya.

Mshirikishi wa eneo la Rift-Valley George Natembeya, alisema maafisa kutoka wizara ya elimu wamepelekwa eneo hilo kukusanya takwimu kuhusu shule zilizoathiriwa, na takwimu hizo zitatumiwa na ngazi zote mbili za serikali katika utafutaji wa suluhisho la kudumu.

Also Read
Saitoti Torome: Athari za Covid-19 zilidumaza ukuaji wa uchumi wa Kenya

Baadhi ya shule zilizoathiriwa ni kama vile Loruk, Sokotei, Ng’ambo, Kiserian, Salabani na pia shule za msingi na Sekondari za Lake Baringo.

Shule nyingine ni kama vile Ng’enyin, Noosukro, Rugus, Lorok, Leswa, Sintaan pia shule ya msingi Lake Bogoria.

Akiongea baada ya ziara ya ukadiriaji kwenye taasisi hizo zilipokuwa zikifunguliwa upya, Natembeya alisema kwamba wanafunzi wote kutoka shule moja ya msingi huko Marishioni kaunti ndogo ya Njoro, ambayo vifaa vyake viliporwa wakati wa kufurushwa kwa wale waliovamia maeneo ya mashariki mwa msitu wa Mau, wamehamishiwa katika shule ya msingi ya Daraja iliyoko karibu.

Also Read
Wavulana 4,000 wakosa kurejea shule huko Baringo baada ya kupashwa tohara

“Nimeagizwa kuhakikisha wakuu wote wa shule za msingi na upili wanakabidhi afisi yangu orodha ya wanafunzi wote wa taasisi zao kabla ya kuzuka kwa Covid-19 na orodha ya wale waliofungua shule,” alisema Natembeya.

Takwimu za idara ya elimu katika kaunti hiyo zinaonyesha kwamba jumla ya vituo 22 vya elimu vimeathiriwa na hali ya mafuriko kwenye kaunti ndogo za Baringo Kaskazini na Kusini.

Also Read
Serikali kuwasaka majangili katika kaunti ya Laikipia

Wakati huo huo Natembeya alisikitika kuwa baadhi ya shule za kibinafsi huenda sizifunguliwe tena baada shule hizo kubadilishwa na kuwa biashara zingine.

Hata hivyo alisema shule za umaa zina uwezo wa kuwakimu wanafunzi ambao wataathirika na hatua hiyo.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi