Wanafunzi wa kidato cha kwanza waanza kuripoti shuleni

Watahiniwa waliofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka uliopita wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza kuanzia Jumatatu tarehe mbili mwezi huu wa Agosti.

Ingawa serikali imepunguza karo za shule za bweni kutokana na kalenda fupi ya masomo na huku wanafunzi wakifurahia kurejea shuleni kuendelea na masomo yao, wazazi wamesema wanashindwa kumudu karo za watoto wao kutokana na ongezeko la gharama ya maisha na changamoto za kiuchumi zinazosababishwa na janga la Covid-19.

Also Read
Wizara ya Afya yaripoti visa vipya 83 vya maambukizi ya korona

Zaidi ya wanafunzi milioni moja watajiunga na kidato cha kwanza kuanzia tarehe mbili mwezi huu ambapo itakuwa na mara ya kwanza kwa wanafunzi wote milioni tano kuwa shuleni tangu kuvurugika kwa masomo hapa nchini kutokana na janga la Covid 19.

Also Read
Ruto asitisha mikutano yake ya kisiasa kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19

Hata hivyo wadau wa sekta ya elimu wamesema hali ya kiuchumi huenda ikasababisha wazazi wengi kushindwa kulipa karo za watoto wao.

Also Read
Magari ya uchukuzi wa umma yaanza kubeba Idadi ya kawaida ya abiria

Kalenda ya masomo ya mwaka huu itakuwa fupi ikilinganishwa na hapo awali kwa kuwa itakuwa na wiki 30 badala ya wiki 39.

Mnamo mwaka 2020 kalenda ya masomo hapa nchini ilisambaratishwa baada ya kuzuka kwa viru vya Covid-19 vilivyosababisha shule kufugwa kwa takriban miezi tisa.

  

Latest posts

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

COVID-19 yavuruga mbinu za upangaji uzazi hapa nchini

Tom Mathinji

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi