Wanafunzi wa kike wapokea msaada wa visodo Kilifi

Mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya Kilifi Getrude Mbeyu ametoa msaada wa visodo zaidi ya 57,000 kwa wanafunzi wasichana ambao walirejelea masomo katika kaunti hiyo.

Mbeyu ametoa visodo hivyo kwa baadhi ya wakuu wa shule hizo katika Chuo Kikuu cha Pwani mjini Kilifi na akawataka wale ambao hawakuhudhuria hafla hiyo watembelee afisi yake ili wachukue mgao wa shule zao.

Amesema kuwa wasichana wa darasa la nane na kidato cha nne wanafaa kutunzwa vyema huku wakijitayarisha kwa mitihani ya kitaifa mwakani, akihoji kuwa wengi kati yao wanatoka familia maskini hasa katika maeneo ya Ganze, Magarini na Kaloleni.

Also Read
Joho, Kingi waanzisha mchakato wa kuunganisha Pwani kabla uchaguzi mkuu wa 2022

“Wasichana wengi wameacha shule baada ya likizo ndefu iliyosababishwa na janga la COVID-19 iliyosababisha ongezeko la visa vya mimba za mapema na dhuluma za kimapenzi. Wale wachache waliobaki shuleni lazima tuwalinde ili wakamilishe masomo yao,” akasema Mbeyu.

Also Read
Aliyekuwa Mwakilishi Wadi ya Junju afikishwa mahakamani kufuatia mauaji ya watu watatu Kilifi

Mwakilishi huyo pia ameahidi kwamba visodo zaidi vitagawanywa kwa wanafunzi wenye mahitaji katika maeneo yote ya kaunti hiyo wakati shule zitakapofunguliwa kikamilifu kwa madarasa yaliyosalia.

Ametoa wito kwa wadau wa sekta ya elimu kufanya mpango wa ufuatilizi wa wanafunzi ambao hawajarejea shuleni licha ya kuwa katika madarasa yaliyoagizwa kurejea juma lililopita.

“Tumepokea ripoti kutoka kwa Mkurugenzi wa Elimu kwamba asilimia 18 ya wanafunzi wa darasa la 8, asilimia 20 ya wanafunzi wa gredi ya 4 na asilimia 17 ya wanafunzi wa kidato cha 4 hawajarejea shuleni. Hii ni ishara kwamba serikali inafaa kuchukua hatua ili kuwanasua,” akaongeza.

Also Read
Watu 190 zaidi waambukizwa Covid-19 humu nchini

Mbeyu pia ametoa msaada wa mashine 104 za kushonea nguo kwa wanafunzi wenye ulemavu katika vyuo mbali mbali vya ufundi na akawataka wale ambao hawajajiandikisha kwenye Baraza la Kitaifa la kushughulikia walemavu wafanye hivyo ili maslahi yao yaangaziwe.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi