Wanafunzi waliojifungua watakiwa kurejea shuleni

Kamishna wa kaunti ya Kitui Thomas Sankei amewataka wanafunzi wote waliojifungua kurejea shuleni baada ya shule kufunguliwa kwa kalenda ya masomo ya mwaka 2021.

Hatua hiyo ni njia mojawepo ya kuhakikisha kwamba asili mia 100 ya wanafunzi wa shule za msingi wanajiunga na zile za upili.

Also Read
Watu wengine 931 waambukizwa COVID-19, wagonjwa 333 wapona huku 6 wakifariki

Akiongea  kwenye afisi yake mjini Kitui siku ya Jumatatu, Sankei alisema kuwa ushirikiano baina ya sekta tofauti zimezaa matunda kwa kuhakikisha kuwa asili mia 98 ya waliofanya mtihani wa darasa la nane,  wanajiunga na shule za upili.

Also Read
Kenya yanakili visa 788 vipya vya COVID-19

Mtawala huyo aliongeza kuwa takriban wasichana 1,000 katika kaunti ya Kitui, waliopachikwa mimba baada ya shule kufungwa kufuatia kuzuka kwa virusi vya Corona mwezi Machi mwaka jana, wamerejelea masomo baada ya kujifungua.

Mwezi Agosti mwaka jana, ripoti ya idara ya watoto katika kaunti ya Kitui, ilionyesha kuwa kaunti hiyo ilinakili visa 3, 207 vya wanafunzi kati ya umri wa miaka 10 na 19 walipachikwa mimba wakati shule zilifungwa baada ya kuzuka kwa virusi vya Corona.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi