Wanafunzi watatu wafariki katika ajali ya barabarani kaunti ya Murang’a

Wanafunzi watatu wa shule ya upili ya wasichana ya Chogoria katika kaunti ya Tharaka Nithi walifariki Jumamosi asubuhi baada ya gari la uchukuzi wa umma walilokuwa wakisafiria kugongana na lori.

Ajali hiyo ambayo ilitokea dakika chache kabla ya saa moja asubuhi katika sehemu ya Kambiti kwenye barabara ya Kenol-Sagana pia ilisababisha kifo cha dereva wa matatu hiyo.

Also Read
Afisa wa polisi mlawiti akamatwa Tharaka-Nithi

Dereva huyo na utingo wa lori hilo pamoja na wanafunzi wengine kadhaa waliokuwa kwenye matatu hiyo, walipelekwa katika hospitali mbali mbali katika kaunti za Murang’a na Kiambu kwa matibabu.

Also Read
Justin Muturi: EACC ilijaribu kuhujumu safari yangu ya Ikulu
Lori lililogongana na matatu hiyo katika eneo la Kambiti. Picha na KNA

Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Murang’a Kusini Alexander Shikondi, alisema dereva wa matatu hiyo alikuwa akijaribu kulipita gari jingine ambapo aligonga lori lililokuwa likisafirisha mazao.

“Abiria wengi katika matatu hiyo walikuwa wanafunzi waliokuwa wakielekea Nairobi. Tumepeleka mili hiyo katika chumba cha kuhifadhi maiti cha General Kago mjini Thika, tunapojaribu kuwasiliana na familia,” alisema Shikondi.

Also Read
COVID-19: Kenya yanakili visa vipya zaidi ya elfu

Shikondi aliongeza kuwa sehemu ya barabara ambapo ajali hiyo ilitokea inaendelea kujengwa huku akitoa wito kwa madereva kuwa waangalifu. Magari hayo yaliyobondeka yalikokotwa hadi katika kituo cha polisi cha Makuyu.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi