Wanajeshi washikwa mateka na wagema Mvinyo Kasarani

Tusker Fc wameweka hai matumaini ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Kenya baada ya kuwashinda wanajeshi Ulinzi Stars goli 1 bila jawabu katika mechi iliyosakatwa Ijumaa alasiri katika uwanja wa Kasarani.

Also Read
Mabondia wa Kenya waanza kwa ushindi Africa Zone 3

Bao la pekee na la ushindi kwa Tusker lilipachikwa kimiani na Boniface Muchiri katika dakika ya 51 ,ukiwa ushindi wa 11 kwa Tusker Fc msimu huu ,wakirejelea ushindi baada ya kupoteza mechi ya pili dhidi ya Bidco United wiki iliyopita.

Also Read
Mbio za Newyork City Marathon zarejea huku zikiandaliwa Novemba 7 mwaka huu

Tusker waliopiga mechi 15 wamezoa alama 35 wakifuatwa na KCB kwa pointi 26 wakiwa na mechi 2 mkobani.

Also Read
Mshambulizi wa Tusker Fc David Majak ajiunga na Kalmar FF nchini Sweeden kwa mkopo wa miezi 6

Katika mechi nyingne Kariobangi Sharks wamekosa nafasi ya kukwea hadi nambari 2 ligini baada ya kulazimishwa kutoka sare tasa dhidi ya Posta Rangers .

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi