Wanajeshi watatu wa KDF watuzwa kwa ujasiri wao wakati wa shambulizi la Manda

Kikosi cha wanajeshi wa marekani wanaohudumu barani afrika cha US AFRICOM, kimewapa tuzo wanajeshi watatu wa kikosi cha KDF kwa ujasiri wao wakati wa shambulizi lililotekelezwa tarehe tano mwezi Januari mwaka wa 2020 na kundi la kigaidi la Al-Shabaab katika kambi ya kijeshi ya Manda, kaunti ya Lamu.

Mkurugenzi wa oparesheni wa kikosi hicho cha US AFRICOM Meja Jenerali Gregory Anderson, alitoa tuzo kwa kanali Daniel Rotich, Meja Martin Muthaura na Koplo Peter Shikuri, kwa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na shambulizi hilo la Manda, ambapo kuna kambi ya kijeshi ya wanajeshi wa KDF pamoja na maafisa wa kijeshi wa marekani.

Also Read
#MakalaMaalum: Coast Guards waimarisha Ziwa Naivasha

Kanali Rotichambaye kwa wakti huo alikuwa naibu kamanda wa oparesheni ya Fagia Msitu, alitambuliwa kwa juhudi zake za kiufundi za kushirikisha usaidizi wan chi kavu wakati wa makabiliano hayo dhidi ya magaidi hao.

Also Read
Rais Kenyatta azindua ujenzi wa nyumba kwa vikosi vya KDF katika Kambi ya Roysambu

Naye Meja Muthaura, akiwa kamanda wa kikosi cha Alpha alipokea tuzo kwa uwezo wake wa kuunganisha kikosi chake kwa haraka na kuwasaidia wanajeshi wa Marekani angani.

Kwa upande wake, koplo Shikuri alipokea tuzo juhudi zake kuhakikisha maadui hao wanaangamizwa. Juhudi zake zilitajwa kuwa muhimu sana katika uwatokomeza magaidi hao wa Alshabab.

Also Read
Watumishi wa umma wanaowania nyadhifa za Kisiasa hawatahitajika kujiuzulu

Akizungumza katika hafla hiyo, naibu mkuu wa vikosi vya wanajeshi wa KDF Luteni Jenerali Francis Ogolla, alisema KDF inawatambua wanajeshi wake wote walioshiriki katika kukabiliana na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab na kuwataka kudumisha ujasiri huo katika kulinda amani katika kanda hii.

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Majukumu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua yabainishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi