Wanakandarasi watakiwa kukamilisha mabwawa kabla ya mwezi Septemba

Waziri wa ugatuzi  Eugene Wamalwa amewaagiza wanakandarasi wote wanaojenga mabwawa katika kaunti za Turkana, Marsabit na Pokot magharibi kuhakikisha kuwa mabwawa hayo yanakamilishwa kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

Akiongea alipozindua kisima kinachotumia kawi ya jua katika eneo la Lokiriamet katika kaunti ndogo ya  Loima katika kaunti ya Turkana,  Wamalwa aliwaambia maafisa wa serikali ya kitaifa na serikali za kaunti husika kuwaharakisha wanakandarasi hao na kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kufikia mwezi September.

Alisema kuwa Rais  Kenyatta na mwenzake wa  Uganda walitia saini mkataba wa makubaliano mwaka wa 2019 ambao utashuhudia Kenya ikijenga mabwawa makuu kama yale yaliyoko katika eneo la Kobebe nchini  Uganda ili kuzuia mizozo ya kung’anga’nia maji.

Alisema kuwa ishara za ukame zimeripotiwa huku akiongeza kuwa mabwawa hayo yatawakinga wakazi kutokana na ukame.

Kisima hicho kilichimbwa na shirika la JICA ambalo liliweka pampu ya kawaida ambayo baadaye iliboreshwa na kufanywa kutumia kawi ya jua na kampuni ya uhandisi ya  Trevcon.

  

Latest posts

Nabulindo ashinda kesi ya kupinga kuchaguliwa kuwa mbunge wa Matungu

Dismas Otuke

Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Ibada ya wafu ya daktari Gakara na wanawe wawili yaandaliwa Nakuru

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi