Wanamgambo 10 wa Alshabab wauawa na maafisa wa KDF Lamu

Takriban magaidi 10 wa kundi la  Al-shabaab ambao wanasemekana walikuwa wakipanga shambulizi kubwa hapa nchini, waliuawa na maafisa wa vikosi vya humu nchini KDF eneo la Lamu.

Katika taarifa, idara ya ulinzi hapa nchini DoD, ilidokeza kuwa ilipata habari kuhusu mpango wa shambulizi hilo, na kuanzisha msako mara moja kati ya eneo la Salila na Kolbio katika msitu wa Boni, na kuwaangamiza magaidi hao ambao wamesajiliwa hivi majuzi katika Kundi hilo la Alshabab.

Also Read
Serikali yaharibu bidhaa ghushi zinazogharimu shilingi milioni 3.3 kaunti ya Garissa

Kulingana na idara hiyo ya  DoD, gaidi mmoja alitoroka akiwa na majeraha.

Also Read
KDF yawalaza wagonjwa kwa matumaini baada ya kuwazawadi Krismasi

“Magaidi hao ni sehemu ya Kundi la Jeysh Ayman linaloongozwa na Maalim Ayman ambaye alikuwa akipanga mashambulizi katika eneo la  LAPSSET,” ilisema taarifa hiyo ya KDF.

Wakati wa oparesheni hiyo, maafisa hao wa KDF walipata roketi ya kurusha gurunedi, silaha kadhaa na  risasi.

Also Read
Majeshi ya Uingereza kuondoa vilipuzi vilivyosalia Laikipia na Samburu

KDF imeapa kuendelea na oparesheni hususan katika mpaka wa Kenya na Somalia pamoja na asasi zingine za usalama katika juhudi za kutokomeza Kundi hilo la kigaidi, linaloaminika kutoka nchini Somalia.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi