Wanamichezo 11 wamepokea hundi za msaada wa masomo Jumatano kutoka kwa kamati ya Olimpiki nchini Kenya NOCK,wanapojiandaa kwa michezo ya Olimpiki ya jijini Paris Ufransa .
Wanaspoti hao walionufaika na msaada huo wa masomo ni Rosafio Danilo wa uogeleaji,Mutua Brian Ndunda wa table Tennis,Mahabila Mathayo Matonya wa Wrestling,Samuel Muturi wa upigaji makasia ,Alexander Kiprotich wa urushaji sagai ,Angella Okutoyi wa Tennis na Josette Njeri wa Triathlon.
Wengine walionufaika na msaada huo wa masomo ni Nancy Akinyi wa uendeshaji baiskeli ,Sharon Wakoli wa Taekwondo,Christine Ongare wa ndondi,na Priscillla Mburu Sports Shooting
Wanamichezo hao wameteuliwa na mashirikisho husika kulingana na matokeo yao na msimamo kwenye msimamo wa dunia.