Wanamuziki wa Nigeria watiwa mbaroni Uganda

Wanamuziki hao Stanley Omah Didia almaarufu “Omah Ley” na Temilade Openiyi maarufu kama “Tems” waliandaa tamasha usiku wa Jumamosi tarehe 12 mwezi Disemba mwaka 2020 mkahawani Ddungu huko Munyonyo, katika jiji kuu la Uganda, Kampala, kinyume na maagizo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Wanamuziki hao wawili, mwandalizi wa tamasha, mmiliki wa sehemu iliyotumika kuandaa tamasha na askari watatu ni kati ya watu tisa waliokamatwa kwa kile kinachosemekana kuwa kosa la kutengeneza mazingira ya msambao wa virusi vya Corona.

Also Read
Siku 40 za mtoto Balqis Isihaka ulimwenguni

Omah Ley alitangaza kutiwa mbaroni kwao kupitia Twitter usiku wa jumapili saa tano naye Tems kabla ya hapo alikuwa amechapisha video ya tukio ikionyesha jinsi watu walikuwa wamejaa kwenye eneo la tamasha huku akishukuru watu wa Uganda.

Polisi walisema waandalizi wa tamasha walianza na vikao vya chakula cha mchana na cha jioni ndio baadaye wakaanza kualika wanamuziki kutumbuiza. Wanalaumiwa pia kwa kushirikiana na polisi wa eneo hilo ili wawape ulinzi.

Also Read
Rais Kenyatta ampongeza Museveni kwa kuhifadhi kiti cha urais nchini Uganda

Naibu msemaji wa polisi wa jiji la Kampala Luke Owoyesigyire alinukuliwa akisema washukiwa wangepimwa virusi vya corona na ikiwa wangepatikana kuwa navyo, hilo lingetumika kama ushahidi dhidi yao kortini.

Picha zilizosambazwa jana zilionyesha wawili hao wakiwa kizimbani huku wanamuziki wengine nchini Nigeria wakianzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kutaka wenzao waachiliwe huru bila masharti yoyote.

Tangu ujio wa Virusi vya Corona, serikali ya Uganda ilipiga marufuku mikusanyiko kama njia moja ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Also Read
Burna Boy na Stefflon Don bado wako pamoja

Agizo hili lilisababisha kukamatwa kwa mwaniaji Urais nchini humo ambaye pia ni mwanamuziki Bobi Wine.

Mwanamuziki huyo baadaye aliachiliwa kwa dhamana, na akaagizwa asiwe anaandaa mikutano ya kisiasa ya watu wanaozidi mia mbili na maagizo ya kuzuia kusambaa kwa Corona yazingatiwe kama vile kuvaa barakoa na kuweka umbali unaostahili kati ya watu.

  

Latest posts

Eduswagga Azungumzia Safari Yake Ya Muziki

Marion Bosire

Tory Lanez Afuta Instagram Kulikoni?

Marion Bosire

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi