Wanaounga mkono BBI wana muda hadi Jumatatu kudhibitisha maelezo yao

WaKenya wana muda wa hadi Jumatatu ijayo kutizama na kubainisha maelezo yote kuwahusu, kwenye orodha ya wale wanao-unga mkono mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020 kupitia kwa mpango wa (BBI).

Katika taarifa kwa vyumba vya habari, mwenyektii wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka humu nchini (IEBC), Wafula Chebukati alihimiza WaKenya kutembelea tovuti ya (IEBC), na kupata orodha ya wale wanao-unga mkono mpango wa BBI ambao majina yao yamethibitishwa.

Also Read
Madereva wa malori wagoma kupinga uchunguzi wa lazima wa Covid-19 Malaba

Chebukati alihimiza wale ambao huenda wakagundua kwamba majina yao yamejumuishwa bila idhini yao kuwasiliana na tume hiyo kwa kumwandikia kaimu katibu wa tume ya (IEBC), kuonyesha pingamizi zao.

Barua hiyo ya malalamishi ikiwa na jina la mlalamishi, nambari yake ya kitambulisho, na pia nambari ya simu  inapaswa kupigwa picha na kutumwa kama barua pepe kwa tovuti ya RPIT@iebc.or.ke au kwa kuwasilisha moja kwa moja kwenye afisi za IEBC zilizoko orofa ya saba ya Jumba la Anniversary Towers Jijini Nairobi.

Also Read
Rais Kenyatta awateua watakaojaza nafasi nne za makamishna wa IEBC

Aidha malalamishi hayo yanapaswa kuwasilishwa kabla ya saa kumi na moja jioni siku ya Jumatatu tarehe 25 Januari mwaka huu wa 2021.

Also Read
Sisi ndio kusema, EACC yaonya kuhusu maadili ya wanaotaka kuwania nyadhifa serikalini

Chebukati alisema majina ya watakaowasilisha malalamishi yao yatafutwa kutoka kwenye orodha hiyo. WaKenya wanaweza kuthibitisha hayo kwa kutazama orodha iliyochapishwa mitamdaoni na tume ya (IEBC).

Kuchapishwa kwa orodha hiyo na hatimaye kipindi cha kuwasilisha malalamiko kunamaanisha safari ya kuelekea kwenye kura ya maamuzi kuhusu mpango wa (BBI) sasa inazidi kukaribia.

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi