Wanariadha watakaoshiriki Kip Keino Classic kubainika Septemba 25

Wanariadha wa Kenya watakaoshiriki  mashindano ya Kip Keino Classic continental tour watabainika ifikiapo Septemba 25.

Kulingana na Rais wa chama cha riadha Kenya Jenerali mstaafu Jackson Tuwei , wanariadha watakaoteuliwa ni wale  waliofanya vyema katika michezo  ya bara afrika  mwaka uliopita nchini Moroko,wale waliowakilisha Kenya katika mashidnano ya dunia mjini Doha Qatar mwaka jana ,wale waliofanya vyema katika mashindano ya kitaifa mwaka uliopita  na wale walio katika nafasi bora kwenye msimamo wa dunia.

Also Read
Bingwa wa dunia Ruth Chepngetich asimulia maisha yake na jinsi alivyoacha shule hadi kunyakua dhahabu ya dunia ya Marathon mwaka 2019

‘’Tufatunga usajili wa wanariadha tarehe 25 mwei huu kisha tutoe start list.Tutatumia michezo ya  All Africa Games mwaka jana,mashindano ya dunia huko Doha Qatar na pia mashindano ya kitaifa mwaka uliopita  na wale walio katika nafasi bora kwenye msiammo wa dunia kuchagua wale watatuwakilisha  katika mashindano ya  Kip Keino Classic’’akasema Rais wa chama cha Riadha Kenya Jackson Tuwei

Also Read
Shujaa yaibuka ya 5 Dubai 7's baada ya kuikwaruza Uganda 36-5

Uwanja wa taifa wa Nyayo ambao utaanda mashindano hayo ya Oktoba 3 unatarajiwa kufunguliwa na rais Uhuru Kenyatta baada ya shughuli ya ukarabati kukamilika .

uzinduzi wa Kip Keino Classic katika makao makuu ya chama cha riadha Kenya

Wanariadha wa Kenya wanatazamiwa kuonyesha umahiri wao katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji wanaume na wanawake ambalo ndilo shindano pekee kwenye ratiba ya mashindano makuu ya mbio.

Also Read
Bingwa wa olimpiki 2008 Wilfred Bungei azungumzia alivyoshinda uraibu wa pombe

Mashindano mengine ambayo wakenya watashirikis ni yale ya Discretionary na National events ambayo yataanza mapema oktoba 3 kabla ya kumalizia kwa mashindano makuu kuanzia saa nane adhuhuri.

Mashindano ya Kip Keino Classic continental tour yalipaswa kaundaliwa Nairobi mwezi Mei lakini yakaahirishwa hadi Oktoba 3 kutokana na janga la covid 19.

 

 

  

Latest posts

Malkia Strikers yafunga mechi za makundi kwa kuilaza Burundi seti 3-0 mashindano ya kuwania kombe la Afrika

Dismas Otuke

Waziri wa zamani wa michezo Hassan Wario afungwa miaka 6 gerezani na kulipa faini ya shilingi milioni 3 nukta 6

Dismas Otuke

Bingwa mara tatu wa dunia Justin Gatlin awasili tayari kushiriki Kip Keino Classic Jumamosi

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi