Wanawake 16 hadi sasa wamechaguliwa katika bunge la kitaifa

Yamkini wanawake 16 hadi sasa wamechaguliwa wabunge kote nchini katika kinyang’anyiro kilichotawaliwa na wanaume.

Aliyekuwa Spika wa Bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi, atakuwa mwanamke wa pekee aliyechaguliwa Jijini Nairobi baada ya kushinda kiti cha eneo-bunge la Dagoretti.

Also Read
Kenya yanakili ongezeko la asilimia 73 la mauzo ya parachichi

Kaunti ya Nakuru itaingia kwenye kumbu kumbu kwa kuwachagua hadi wanawake wa nne kuwakilisha maslahi ya wakaazi wake katika Bunge lijalo la 13.

Miongoni mwa wanawake ambao wamehifadhi viti vyao ni Jane kihara katika eneo-bunge la Naivasha, Alice Wahome wa eneo-bunge la Kandara na Millie Odhiambo wa eneo-bunge la Suba Kaskazini.

Also Read
Kenya yachaguliwa tena katika baraza la uchukuzi wa baharini

Wengine ambao wanaingia bungeni kwa mara ya kwanza ni pamoja na Suzanne Kiamba kwa tiketi ya Wiper ambaye amechaguliwa mbunge wa kwanza mwana-mke katika eneo-bunge la Makueni.

Also Read
Hosea Kiplagat ambaye ni msaidizi wa zamani wa Rais Moi amefariki

Katika kaunti ya Samburu, Naisula Lesuunda amechaguliwa tena kuwa mbunge wa Samburu Magharibi.

Katika kaunti ya Narok, mwana-harakati wa kutetea haki za wanawake Agnes Pareiyo, sasa ndiye mbunge mteule wa eneo-bunge Narok Kaskazini.

  

Latest posts

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

NHIF yaongeza muda wa kuwapa bima ya afya maafisa wa Polisi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi