Wanawake wanaougua Fistula kunufaika na Matibabu bila malipo katika hospitali ya Kenyatta

Zaidi ya wanawake 30 wenye kukabiliwa na nasuri yaani kasoro ya kuvuja mkojo na kinyesi wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji bila gharama na kupewa huduma ya ushauri wa kimatibabu.

Shughuli hiyo itaandaliwa katika kambi ya matibabu itakayidumu wiki nzima  katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta-KNH.

Also Read
Safaricom yafadhili mashindano ya dunia ya riadha kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 kwa milioni 66 nukta 5

Kambi hiyo ambayo imepatiwa jina la Fistula, itaendelea hadi siku ya Ijumaa wiki hii.

Zoezi hilo limeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Wakfu wa Safaricom,shirika la umoja wa mataifa kuhusu mipango ya uzazi-UNFPA, shirika la Flying Doctors la bara la Afrika,Shirika la AMREF Health Africa na mkakati wa Beyond Zero.

Also Read
Kenya yamrejesha nchini mwake mshukiwa wa ulanguzi wa binadamu

Kambi hiyo inafanywa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kukomesha madhara ya nasuri-IDEOF.

Also Read
Jubilee yajiondoa kwenye uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Msambweni

Shughuli hiyo ya matibabu, inalenga kutoa uhamasisho kuhusu matatizo ya nasuri miongoni mwa wanawake,huku washikadau wakijitahidi kupata suluhisho kwa tatizo hilo ifikapo mwaka wa 2030.

  

Latest posts

Kithure Kindiki ajiondoa katika ulingo wa kisiasa

Tom Mathinji

Raila Odinga atangaza sehemu ya baraza lake la Mawaziri

Tom Mathinji

Kalonzo Musyoka asema kwaheri kwa Muungano wa Azimio la Umoja

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi