Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Jimmy Wanjigi ambaye ameelezea nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama cha ODM anasema kuwa taifa hili haliko tayari kiuchumi kuwapa vijana wasiokuwa na kazi shilingi elfu sita kila mwezi kama alivyoahidi kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga iwapo atabuni serikali ijayo.

Akiongea katika kanisa la AIPCA Kutus katika kaunti ya Kirinyaga, Wanjigi alisema kuwa taifa hili linakabiliwa na changamoto nyingi hasa katika kulipa madeni yake huku akisema kuwa itabidi shilingi bilioni 300 zitumike kila mwaka iwapo pendekezo la Raila litatekelezwa.

Also Read
Mahakama ya rufani yaangaziwa huku ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mchakato wa BBI

Alisema swala hilo halitawezekana na vile vile litakuwa ni kama kuwahujumu wakenya wanaofanya kazi kwa bidii.

Alisema Raila anafaa kushinikiza kutekelezwa kikamilifu kwa sheria kuhusu malipo ya uzeeni ambayo inatoa mkakati mwafaka kwa serikali kuwasaidia kifedha wakenya wote wasio na ajira.

Also Read
William Ruto: Kuna muda wa kuafikiana kuhusu BBI

Wanjigi alisisitiza kuwa atawania urais huku akitoa wito wa kufanywa kwa shughuli ya uteuzi ya chama hicho kwa njia ya haki na uwazi.

Kiongozi wa chama cha ODM ambaye bado hajatangaza rasmi azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, hivi majuzi alisema kuwa iwapo atabuni serikali ijayo, atawapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi ili kujimudu.

Also Read
Idadi ndogo ya wapiga kura yashuhudiwa katika uchaguzi mdogo wa Kiambaa

Tangazo hilo la Odinga lilionekana kukabiliana na mfumo unaopendekezwa na naibu rais Dkt William Ruto almaarufu bottom up economy.

Huku uchaguzi mkuu unaponukia, wanasiasa hasaa wanaowania wadhifa wa urais, wamekuwa wakiwauzia sera zao wananchi katika kile ambacho kimeonekana kuwa kampeni za mapema hapa nchini.

  

Latest posts

Kennedy Obuya asimulia jinsi mchezo wa Ckricket ulivyobadilisha maisha yake

Dismas Otuke

Watu 19 wafariki baada ya basi kutumbukia mtoni Kaunti ya Kitui

Tom Mathinji

Watu wawili zaidi wametolewa katika migodi ya Abimbo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi