Nahodha wa Harambee Stars alifunga bao lake la pili Jumapili usiku tangu ajiunge na Montreal Impact huku akiisaidia kupata ushindi wa ugenini wa mabaoi 3-2 katika mchuano w aligi kuu Marekani MLS.
Wanyama lifunga bao hilo kunako dakika ya 74 kwa kichwa kufuatia mkwaju wa kona uliochongwa na kiungo Romel Quiorto ,likiwa bao lake la pili tangu atue kwenye timu hiyo ya Cananda mapema mwaka huu akitokea Tottenham Hotspur.
La marque est égale grâce a @VictorWanyama.
Wanyama rips one into the top corner to tie things up.
2-2 | #DCvMTL | #IMFC pic.twitter.com/2cb7gbx5l3
— CF Montréal (@clubdefootmtl) November 8, 2020
Kiungo huyo ambaye maajuzi alitajwa kuwa miongoni mwa vijana 100 walio na ushawishi mkubwa bara Afrika, atakosa mchuano wa Harambee Stars dhidi ya Comoros Jumatano hii katika uwanja wa Kasarani baada ya kunyimwa ruhusa ya kusafiri.
Ushindi huo uliiwezesha Montreal kumaliza ya 9 katika msimamo wa MLS Eastern Conference kwa pointi 26 kutokana na mechi 23 za msimu huu.
Baada ya msimu wa ligi kuu ya MLS kufikia tamati Jumapili usiku ,Montreal Impact wamepangiwa kuchuana na New England Revolution katike pambano la mchujo Novemba 21.
Kiungo huyo ameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji mgeni bora wa mwaka katika ligi ya MLS na pia kuwania tuzo ya watu wanaofanya shughuli za kuisaidia jamii maarufu kama Works Humanitarian of the Year awards.