Zaidi ya waogeleaji 500 wanatarajiwa kushiriki mashindano ya wazi ya uogeleaji yatakayoandaliwa baina ya Jumamosi na Jumapili hii katika shule ya Regis mtaani Runda.
Kulingana na afisa wa uhusiano mwema wa shirikisho la uogeleaji kaunti ya Kiambu Nesmus Mbati, mashindano hayo pia yatatumika kufuzu kwa mashindano ya kitaifa ya kiwango cha pili na tatu huku yakiwashirikisha wanafunzi wa umri wote kutoka kaunti za Kajiado ,Machakos,Nairobi,,Murang’a,Nyeri na Kiambu.
Kaunti hiyo pia itaandaa mashindano ya level 1 na level 2 katika uwanja wa Kasarani mwezi Machi mwaka huu ,huku waogeleaji bora wakifuzu kwa mashindano ya kimataifa nchini Uganda .
Kama njia ya kukuza vipaji vya uogeleaji ,kaunti ya Kiambu itaandaa mashindano ya uogeleaji kwa umri wote,kando na kuwania kuandaa mojawapo wa mashindano ya kitaifa mwaka huu.