Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Taifa la Kenya lina wawakilishi kwenye vitengo vikubwa vya tuzo za “All Africa Music Awards – AFRIMA” mwaka 2021 ambavyo ni vya bara zima yaani “Continental Categories”.

Wasanii hao ni pamoja na Sauti Sol, Bensoul, Nviiri The storyteller, Xenia na NHP kwa kibao chao kiitwacho “Rhumba Japani” na wanawania tuzo katika kitengo cha ” BEST AFRICAN DUO, GROUP OR BAND”

Khalighraph Jones ameteuliwa kuwania tuzo kwenye kitengo cha “BEST AFRICAN RAPPER OR LYRICIST” kwa kibao chake kiitwacho “Wavy” ambacho amemshirikisha Sarkodie huku mwelekezi Road Man akiteuliwa kuwania tuzo katika kitengo cha “BEST AFRICAN VIDEO” kutokana na kazi aliyoifanya ya kibao cha Nairobi cha Bensoul akiwashirikisha Sauti Sol, Nviiri the Storyteller na Mejja.

Also Read
King Kaka Atoa Kibao Kipya

Nikita Kering ameteuliwa kuwania tuzo kwenye kitengo cha “BEST ARTISTE, DUO OR GROUP IN AFRICAN R&B SOUL” kwa kibao chake “Ex” ambacho pia kimemweka awanie tuzo kwenye kitengo cha “SONGWRITER OF THE YEAR” ambapo anapambana na Bensoul na kibao chake Nairobi.

Also Read
AEAUSA wakamilisha uteuzi

Ali Mukhwana ambaye aliingia kwente ulingo wa muziki kupitia kwa shindano la “Exodus to Stardom” ambalo lilipeperushwa na runinga ya KBC ameteuliwa kuwania tuzo katika kitengo cha “BEST MALE ARTISTE IN AFRICAN INSPIRATIONAL MUSIC” kwa wimbo wake uitwao “Maombi Yangu” huku Noel Nderitu akiteuliwa kuwania tuzo sawia upande wa kina dada kupitia kwa wimbo wake “Enough”.

Also Read
Sauti Sol, Ethic, Khaligraph kwenye tuzo za MAMA

Orodha ya wawaniaji katika vitengo vyote 40 vya tuzo za AFRIMA ilizinduliwa rasmi tarehe 22 mwezi Septemba mwaka huu wa 2021 na shughuli ya kupiga kura itaanza tarehe 27 mwezi Septemba ikamilike tarehe 20 mwezi Novemba mwaka 2021. Sherehe ya kutuza washindi itafanyika baadaye jijini Lagos nchini Nigeria.

Waandalizi wanasema kwamba walipokea maombi ya nyimbo zipatazo 8 880 lakini wakachuja zikabakia nyimbo kama 400 hivi kwa ajili ya tuzo hizo.

  

Latest posts

Arrow Bwoy Amefiwa

Marion Bosire

Shona Ferguson Ashinda Tuzo Hata Baada Ya Kifo

Marion Bosire

Snoop Dogg Atangaza Kifo Cha Mamake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi