Wasanii wapata Fursa kwenye maonyesho ya SabaSaba

Kwa mwaka wa pili mfululizo wasanii wa nchi ya Tanzania ambao pia ni wajasiriamali wamepata fursa ya kuonyesha bidhaa zao kwenye maonyesho ya kibishara ya sabasaba katika viwanja vya sabasaba nchini Tanzania.

Haya yamewezeshwa na mpango kwa jina “Meet Your Star” ambao unaendeshwa na mwanahabari Zamaradi Mketema ambaye pia ni mmiliki wa Zamaradi Tv.

Also Read
Meghan Markle na Prince Harry kuandaa filamu

Zamaradi alianzisha eneo linalofahamika kama “Banda la Mastaa” kwenye maonyesho hayo mwaka jana kwa nia ya kuwapa wasanii wa muziki, waigizaji, wachekeshaji na wengine nafasi ya kuuza bidhaa zao kazi ambayo wanaifanya kando na sanaa.

Mwaka huu wa 2021, Meet Your Star ilizinduliwa rasmi na mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo ambaye alishukuru Zamaradi kwa kumpa heshima ya kuzindua tukio hilo.

Also Read
Happy Birthday Shihi Baby!

Wasanii ambao wako pale kwa ajili ya kuonyesha bidhaa zao ni kama vile Shilole ambaye anaonyesha Shishi Foods na Irene Uwoya ambaye anauza bidhaa za kutunza ngozi na za urembo kati ya wengine wengi.

Kwa hivyo mashabiki wao wanapata nafasi ya kutangamana nao na kujua wanachofanya zaidi ya kuwapa burudani na ikiwezekana wawe wateja wao.

Also Read
Natamani kuimba na Christina Shusho - Donat Mwanza

Wasanii wengine ambao hawana bidhaa za kuuza pia wamekuwa wakifika kwenye maonyesho hayo ya sabasaba na hasa banda la mastaa kwa ajili ya kukutana na mashabiki wao. Wanajumlisha waigizaji wa filamu za Bongo kama vile Aunt Ezekiel, Kajala Masanja na wengine wengi.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi