Washiriki wote wa kongamano la Ugatuzi sharti wawe wamechanjwa dhidi ya Covid-19

Wale wote watakaoshiriki katika kongamano kuhusu ugatuzi katika kaunti ya Makueni, watahitajika kuwa wamechanjwa dhidi ya virusi vya Covid-19.

Siku ya Ijumaa, Baraza la magavana (COG) liliashiria kuwa  utoaji wa chanjo ndio njia muhimu zaidi kuhakikisha usalama wa watakaohudhuria  Kongamano hilo huku kiwango cha maambukizi cha ugonjwa wa Covid19 kikiongezeka.

‘‘Mkutano huu ni wa ana kwa ana na wala sio  kupitia mtandao. Masharti ni kwamba kila mshirika anapaswa kuwa amechanjwa dhidi ya Covid-19,” alisema naibu mwenyekiti wa baraza la magavana James Ongwae

Also Read
Ukusanyaji saini za BBI kuanza rasmi leo

Ili kuhakikisha hayo yanaafikiwa, Ongwae alidokeza kuwa mipango imewekwa kupeleka chanjo zaidi katika kaunti ya Makueni kuhakikisha wadau wote wanachanjwa kabla ya makala ya saba ya kongamano hilo kuhusu ugatuzi.

Ongwae aliyasema hayo mjini Wote kaunti ya Makueni akiwa katika ziara ya ukaguzi wa maandalizi ya kongamano hilo litakaloanza tarehe 23 hadi tarehe 26 mwezi Agosti katika shule ya upili ya wavulana ya Makueni.

Also Read
Serikali ya Kaunti ya Embu yawarejesha kazini wafanyikazi 1,200 wa Afya

Kwa mujibu wa gavana Ongwae kati ya washiriki  5,000 na 6,000 wanatarajiwa watahudhuria kongamano hilo.

Ongwae alisema kuwa Rais Uhuru Kenyatta, naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga, watahudhuria kongamano hilo.

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana aliwahakikishia wageni wote kuwa kila kitu Kiko tayari katika muda huo wote watahudhuria kongamano hilo.

Also Read
Shule za Garissa ziko tayari kwa ufunguzi, wasema Wakuu wa Elimu

” Tuko tayari kuandaa kongamano hilo, tunazidi kuimarisha hali ya malazi na kuhakikisha hakutakuwa na uhaba wowote. Vile vile tunatarajia biashara katika eneo hili zitaimarika wakati wa kongamano hilo,” alisema Kibwana.

Alielezea haja ya kuwa na mikutano ya pembeni kuhakikisha mashirika ya mashinani na yale ya kijamii yanajumuishwa katika vita dhidi ya ufisadi.

  

Latest posts

Vifo vya ndugu wawili vyazua taharuki Embu Kaskazini

Tom Mathinji

Gladys Erude ameaga dunia

Marion Bosire

Cheruiyot, Simotwo na Kipsang kushiriki nusu fainali ya mita 1500

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi