Washukiwa wa Alshabab watekeleza shambulizi katika eneo la Majengo kaunti ya Lamu

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki, baada ya majambazi waliojihami, ambao wanashukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab, kuvamia eneo moja la ujenzi, na kushambulia kwa risasi eneo la Majengo katika kaunti ya Lamu Alhamisi usiku.

Kulingana na maafisa wa polisi, waathiriwa walioangamia wanahusisha wafanyikazi waliokuwa wakijenga barabara kuu ya kutoka bandari ya Lamu hadi nchini Ethiopia na Sudan kusini.

Also Read
Shule katika kaunti ndogo ya Lamu Magharibi zaamrishwa kufunguliwa

Inaarifiwa kwamba majambazi hao pia waliteketeza gari moja la ujenzi na pikipiki.

Wanamgambo hao kisha waliwateka nyara raia wawili wa China na baadaye wakamwachilia mmoja baada ya kumjeruhi vibaya.Washambuliaji hao pia waliharibu daraja moja lililokuwa likijengwa katika eneo la Majengo-Omolo.

Also Read
Wavuvi kutoka Lamu wapinga uamuzi wa mahakama ya ICJ kuhusu mpaka wa baharini

Shambulizi hilo linajiri siku mbili tu baada ya vikosi vya ulinzi humu nchini, kumuua kwa kumpiga risasi mwanamgambo mmoja wa kundi la Alshabab katika kaunti hiyo la lamu, huku wanamgambo wengine wakitoroka na majeraha ya risasi.

Also Read
Mvua kubwa kuendelea kushuhudiwa humu nchini

Inaaminika wanamgambo wa Alshabab wamejificha katika msitu wa boni, huku vikosi vya asasi mbali mbali za usalama zikijizatiti kuhakikisha wanamgambo hao wanatokomezwa kikamilifu.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Kenya kukabana koo na Puerto Rico mechi ya mwisho ya kundi A mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi