Washukiwa wa shambulizi la Westgate kujua hatma yao juma lijalo

Washukiwa wa shambulizi la kigaidi la Westgate, sasa watajua hatma yao Ijumaa juma lijalo baada ya mahakama kuahirisha kesi hiyo.

Hii ni baada ya afisa wa urekebishaji tabia Peter Macharia kuiambia mahakama kwamba ripoti ya kabla ya kuhukumiwa kwao haijakuwa tayari, kwani baadhi ya wahasiriwa bado hawajahojiwa.

Also Read
Chama cha Ekeza chawafidia wanachama wake pesa walizowekeza

Afisa huyo anasema waliweza kuwahoji washukiwa wawili, Mohammed Ahmed Abdi na Hussein Hassan Mustafa, lakini bado hawajazungumza na jamaa za watuhumiwa, na pia mmoja wa wahasiriwa wa shambulizi la kigaidi la Westgate lililotekelezwa na wanamgambo wa Al-shabaab mnamo mwaka wa 2013.

Also Read
Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Amesema ripoti hiyo itakuwa tayari juma lijalo, ili kumwezesha hakimu kutoa hukumu ifaayo.

Hakimu Mkuu Francis Andayi amewaagiza waandishi wa habari kutoandaka chochote kuhusu taarifa za maumivu ya wahasiriwa ambazo zimewasilishwa kotini.

Also Read
Washukiwa wa lile shambulizi la Westage wafikishwa mahakamani Jijini Nairobi

Mapema mwezi huu, Hakimu Andayi aliwapata washukiwa hao wawili na hatia ya kushiriki njama za  kutekeleza shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 67 na wengize zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Hata hivyo mtuhumiwa mwingine kwa jina Abdullahi Omar aliachiliwa huru kwa ukosefu wa ushahidi.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi