Washukiwa watatu wa ugaidi wanaswa kaunti ya Garissa

Washukiwa watatu wa ugaidi wamekamatwa katika eneo la Lagdera, Kaunti ya Garissa na silaha kupatikana kutoka kwao.

Watatu hao walipatikana na  bunduki  nane aina ya AK-47, risasi 2,004, magazini  8 na lita 20 za petroli.

Kamishna wa  eneo la  Kaskazini Mashariki, Nicodemus Ndalana, alisema polisi kwenye eneo la  Lagdera walikuwa wakishika doria katika  barbaara ya  Baraki-Maalmin,  walipowaona watu hao watatu wakiwa na gari ndogo jeupe aina ya Toyota   lenye  nambari ya  usajili KCY 953L.

Washukiwa hao walitambuliwa kama Abdirizack Mohamed  mwenye umri wa miaka 24, Jimale Abey Mahamud mwenye umri wa miaka 21 na Nur Ibrahim Alasow mwenye umri wa miaka 30.

Ndalana alisema tayari uchunguzi unaendelea ili kubaini watuhumiwa hao walikuwa wanatoka wapi, na nia  ya  silaha hizo.

Wakati huo huo,  alionya kuwa  wanasiasa wanaopanga kufadhili mapigano ya  kiukoo au mipaka kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao  watachukuliwa hatua.

Kwa upande wake, kamanda wa polisi wa  eneo hilo,  Rono Bunei alisema kuwa mtu yeyote atakayepatikana kuwa na hatia ya kuwasaidia     washukiwa hao kwa njia yoyote, atachukuliwa kama mshukiwa wa ugaidi na atakabiliwa na nguvu kamili ya sheria bila kujali tabaka lake katika  jamii.

  

Latest posts

Rais Kenyatta amwomboleza Nancy Karoney, dadake waziri wa ardhi Farida Karoney

Tom Mathinji

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi