Washukiwa watatu wa utekaji nyara wakamatwa na Polisi Githurai

Polisi wamewatia mbaroni washukiwa watatu wa utekeji nyara ambao walikuwa wamemteka nyara mwanaume mmoja wa umri wa miaka 23 kwenye nyumba ya chumba kimoja mtaa wa Githurai hapa Nairobi siku ya Jumanne.

Walikuwa wameitisha fidia ya shilingi 300,000 kutoka familia yake kabla ya kumuachiliwa huru.

Also Read
Gavana wa Laikipia Nderitu Muriithi alalamikia ongezeko la stakabadhi bandia za ardhi

Polisi walisema mwathiriwa huyo alikuwa amesafiri kutoka Mwingi Mashriki hadi Githurai ili kuwazuru wachumba wanaotoka kijiji kimoja naye ila alipowasili alimpata mwanamke akiwa kwa nyumba peke yake.

Also Read
DCI yawakamata washukiwa wanaolaghai watu kwa kigezo cha kuwatafutia wapenzi

Walisema mumewe alifika nyumbani akiandamana na wanaume wengine watatu ambao walimvamia mwathiriwa huyo kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.

Walichukua shilingi 5,000 kutoka kwake kabla ya kumpeleka kwa chumba kimoja kisicho na kitu.

Also Read
Kuna matumaini ya kuimarika kwa sekta ya utalii hata baada ya msimu wa sherehe

Mwathiriwa huyo alilazimishwa kuwasiliana na familia yake ili kuitisha fidia huku wakitishia kumdhuru endapo familia yake itakataa kutoa fidia .

Familia yake iliripoti kisa hicho kwa polisi ambao walimsaka hadi mahali alipokuwa na kuwakamata watatu hao.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi