Washukiwa wawili wa mauaji ya Herman Rouwenhourst kuzuiliwa kwa siku 21 zaidi

Washukiwa wawili wa mauaji ya mfanyi biashara Herman Rouwenhourst, ambaye ni raia wa Uholanzi mwenye makao yake mjini Mombasa pamoja na mlinzi wake, wamezuiliwa kwa siku 21 zaidi kutoa nafasi ya kukamilishwa kwa uchunguzi.

Timothy Omondi al maarufu Mohammed Khalid na Mercy Masika, wanatuhumiwa kwa kumuua mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 55 nyumbani kwake katika eneo la Shanzu, kaunti ya Mombasa mwezi uliopita.

Hakimu mkuu mwandamizi David Odhiambo aliagiza kwamba Omondi mwenye umri wa miaka 22 na Masika mwenye umri wa miaka 33 wazuiliwe kwenye korokoro za vituo vya polisi vya Bamburi na Nyali mtawalia wakati uchunguzi ukiendelea.

Also Read
Wakazi wa Mombasa wakashifu utumizi wa daraja la Liwatoni

Afisa anayeongoza uchunguzi wa mauaji hayo Reuben Mwaniki amesema washukiwa walipatikana mafichoni mwao kwenye nyumba mpya iliyojengwa kwenye kipande cha ardhi kilichonunuliwa hivi majuzi.

Afisa huyo alidokeza kuwa maafisa wa polisi wanachunguza pia iwapo pesa zilizotumika kununua kipande hicho cha ardhi, ziliibwa kutoka kwa marehemu baada ya mauaji hayo.

Also Read
Afisa wa polisi akamatwa kuhusiana na mauaji ya utingo

Wachunguzi hao walisema kiasi kisichojulikana cha fedha za sarafu za humu nchini na za kigeni ziliibwa kutoka kwa nyumba ya marehemu.

Polisi walitaka wapewe muda zaidi kuwatafutia waliouza kipande hicho cha ardhi ili kuandikisha taarifa kwa polisi pamoja na kuwasilisha stakabadhi za ununuzi wa ardhi hiyo.

Wakati wa kutiwa nguvuni kwa washukiwa hao, polisi walipata risasi moja, ganda moja la risasi, pingu, viatu na nguo zilizokuwa na damu, simu kadhaa za mkononi pamoja na kadi kadhaa za simu.

Also Read
Mwanaume auawa Kitui baada ya kufumaniwa kwenye ‘tendo’ na ng’ombe

Vitu hivyo vilivyopatikana vitatumiwa kama ushahidi huku uchunguzi ukitarajiwa kufanywa kubainisha ikiwa damu ilivyokuwa katika vitu hivyo unaambatana na Ile ya marehemu.

Riziki Cherono, ambaye ni mke wa mwendazake alifikishwa mahakamani mwezi uliopita kuhusiana na mauaji hayo. Idara ya DCI ilitaka iruhusiwe kumzuilia kwa siku. Hata hivyo anatarajiwa kuitikia shtaka hilo.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi